Girl Shine ya UN Women imenijengea kujiamini na sasa nasaidia familia yangu- Rachael
Listen now
Description
Mizozo na umaskini wa kupindukia kwenye mazingira ya uhitaji mkubwa wa msaada wa kibinadamu huwaweka wasichana katika hatari kubwa ya kukumbwa na ukatili na kunyanyaswa. Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake, UN WOMEN kwa kutambua hilo linatekeleza miradi katika kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma nchini Kenya ili kuwajengea uwezo wasichana barubaru ili hatimaye waweza kuandaa mustakabali bora wa maisha yao. Girls Shine ni moja ya miradi hiyo kupitia mradi mkubwa wa LEAP unaoungwa mkono na serikali ya Japan tangu mwaka 2018. Wasichana wakimbizi na wenyeji wananufaika na mradi huu na sasa wanapaza sauti kama katika Makala hii iliyoandaliwa na UN Women barani Afrika na kusimuliwa na Thelma Mwadzaya.
More Episodes
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tunakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako mapigano yanayoendelea yanatenganisha watoto na familia zao na sasa hatua zinachukuliwa kuunganisha watoto na familia zao. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zinazohusiana na janga la...
Published 02/07/23
Pamoja na kwamba juhudi zinaendelea duniani kote kutokomeza mila iliyopitwa na wakati ya ukeketaji, takwimu za Umoja wa Mataifa bado zinaonesha kuwa takribani watoto wa kike milioni 4.2 duniani wako hatarini kukeketwa mwaka huu wa 2023 pekee. Hata hivyo ni harakati za wadau mbalimbali kushiriki...
Published 02/06/23