29 NOVEMBA 2022
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tukiangazia juhudi za kuwajengea watoto tabia ya kupenda kusoma vitabu na pia habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya UNAIDS na WHO, na usaidizi kwa wakimbizi na jamii za wenyeji nchini Chad. Mashinani tutakwenda nchini Cameroon, kulikoni? Msichana Marynsia Mangu kwa kutambua umuhimu na maarifa yanayopatikana kwenye vitabu lakini jitihada zake za kuwashawishi marafiki zake kusoma vitabu kushindwa kuzaa matunda akaamua kufuata usemi wa Kiswahili Samaki mkunje angali mbichi na kuanzisha shirika la success Hands au kwa lugha ya Kiswahili Mikono yenye Mafanikio ambalo jukumu lake ni kuwajengea watoto tabia yakupenda kusoma vitabu tangu wangali tumboni mwa mama zao.Ripoti mpya ya tathimini iliyofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masiuala ya ukimwi UNAIDS kuelekea siku ya ukimwi duniani ambayo kila mwaka huadhimishwa Desemba Mosi inaonyesha kuwa pengo la usawa ni kikwazo kikubwa katikia juhudi za kutokomeza janga la ukiwmi duniani. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO leo limesema majeraha na machafiuko vinasababisha vifo vya watu 12,000 kila siku kote duniani ambavyo ni sawa na kifo 1 kati ya vifo 12. Kupitia ripoti yake mpya “Mtazamo wa kuzuia majeraha na machafuko” iliyotolewa leo mjini Geneva Uswis WHO inasema sababu kuu tatu kati ya tano zinazosababisha vifo vywa watu wa umri wa kati ya miaka 5 hadi 29 ni majeraha, athari za ajari za barabarani , mauaji na kujiua.Na mashirika ya Umoja wa Mataifa ile la Mpango wa chakula duniani WFP na linaloshughulika na wakimbizi UNHCR wametoa ombi la dola milioni 161 ili wasikatishe huduma ya chakula cha msaada kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi na jamii za wenyeji nchini Chad.Na leo mashinani tutaelekee barani Afrika nchini Cameroon kumsikiliza Cecile Ndjebet ambaye anaeleza uhusiano uliopo kati ya haki ya umiliki wa ardhi hasa kwa wanawake na uhifadhi wa mazingira.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
More Episodes
Sudan Kusini ni moja ya nchi iliyoathirika kwa muda mrefu na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo mara kwa mara makundi ya wapiganaji wenye silaha yalikuwa yakivamia katika vijiji na kuwaua raia na kupora mali zao. Kutokana na sababu hiyo wananchi wengi wamekuwa wakikimbilia katika kambi za...
Published 02/01/23
Mawaziri wa afya na wawakilishi kutoka nchi 12 za Afrika na wadau wa kimataifa leo wameahidi na kuweka mipango ya kutokomeza ukimwi miongoni mwa watoto ifikapo mwaka 2030,  limesema shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na kutokomeza VVU na ukimwi UNAIDS. Ahadi hiyo imetolea jijini Dar es...
Published 02/01/23