Makaburi ya wayahudi mjini Fez nchini Morocco, ushahidi wa jamii tofauti kuishi pamoja kwa amani
Listen now
Description
Umoja wa Mataifa unasema robo tatu ya migogoro mikuu ya ulimwengu ina uhusiano na masuala ya kitamaduni na kwa hivyo kuziba pengo kati ya tamaduni ni jambo la haraka na la lazima kwa ajili ya amani, utulivu na maendeleo. Makaburi ya Kiyahudi huko Fez, Morocco ni ushuhuda wa utamaduni tofauti kuishi pamoja kwa amani. Wakiwa katika safari ya kikazi huko Fez, kuangazia Mkutano wa tisa wa Jukwaa la Umoja wa Mataifa la Muungano wa Ustaarabu, UNAOC, May Yacoub na Alban Mendes De Leon kutoka Timu ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa walikutana na Johanna Devico Ohana, mzaliwa wa Fez, ambaye anatunza makaburi haya yenye umri wa miaka 200, akiheshimu jina la marehemu babake ambaye mwenyewe alikuwa msimamizi wa utunzaji wa makabuli haya hadiĀ  alipoaga dunia miezi michache iliyopita. Anold Kayanda anasimulia makala hii kwa lugha ya Kiswahili.
More Episodes
Hii leo jaridani utasikia kuhusu ushirikishwaji wa vijana katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Maendeleo UNDP. Pia utasikia muhtasari wa habari kuhusu wasaka hifadhi huko nchini Uingereza kuhamishiwa Rwanda, Makaburi ya halaiki huko Gaza na...
Published 04/23/24
Katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, afisa mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) anayehusika na masuala ya dharura na mnepo, Rein Paulsen ametahadharisha kuwa hatari ya kutokea baa la njaa nchini Sudan ni halisi na kwa hivyo wakati wa kuchukua hatua ni...
Published 04/22/24