Guterres atoa onyo kuwa hatuwezi kutatua zahma zinazotukabili katika dunia iliyogawanyika bila mshikamano
Listen now
Description
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia haiwezi kutatua changamoto kubwa inazokabiliwa nazo hivi sasa kuanzia mabadiliko ya tabianchi, vita ya Ukraine, mdororo wa uchumi na athari zinazoendelea za janga la COVID-19 katikia hali ya sasa ya mgawanyiko na kutokuwa na mshikamano hivyo wakati wa kufumbia macho changamoto hizi umepita na wanaochangia wawajibishwe. Katibu Mkuu Guterres ameyasema hayo mjini Davos Uswis katika hotuba yake kuhusu hali ya dunia kwenye siku ya pili ya jukwaa la uchumi duniani akibainisha kwamba wakati dunia inahitaji ushirikiano zaidi katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi , upunguzaji wa mzigo wa madeni na afya uya kimataifa kuna mgawanyiko na changamoto inaongezeka linapokuja suala ya vita ya Ukraine  akisema "Hasa uvamizi wa Urusi kwa Ukraine sio tu kwa sababu ya mateso yasiyoelezeka kwa watu wa Ukraine, lakini kwa sababu ya athari zake kubwa za kimataifa kwa bei ya chakula na nishati, kwenye minyororo ya biashara na usambazaji na maswala ya usalama wa nyuklia, kwa misingi hiyo hiyo ya sheria za kimataifa”.  Akisisitioza kuhusu suala la mabadiliko ya tabianchi amelaani makampuni makubwa ya mafuta kwa kupuuza sayansi kuhusu mabadiliko ya tabianchi, na kushutumu sekta ya mafuta na gesi kwa kutafuta kupanua zaidi wigo wa uzalishaji licha ya kujua kwamba kwamba mtindo wao wa biashara hauendani na maisha ya binadamu.   Amesema"Baadhi ya makampuni makubwa ya mafuta wanadanganya kwa kiasi kikubwa na kama vile ilivyo kwa sekta ya tumbaku, wale wanaohusika kuchochea mabadiliko ya tabianchi lazima wawajibishwe."  Pia amezungumzia migawanyiko ikiwemo baina ya Mashariki na Magharibi hasa Marekani na Uchina hususan katika suala la haki za binadamu na usalama wa kikanda na Kaskazini na Kusini ambao amesema hashawishiki kwamba Kaskazini inatambua kiwango cha madhila yanayowakabili watu wa Kusini hasa linapokuja suala la afya kuhusu usawa wa usambazaji wa chanjo.  Amehitimisha hotuba yake kwa kutoa wito kwa serikali zote, sekta binafsi na wadau wote kuunda njia za ushirikiano zaidi, ikisisitiza haja ya kuziba pengo la migawanyiko yote kwa kurekebisha na kujenga usawa katika mfumo wa fedha wa kimataifa, Kuchukua hatua za maana dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, Kurekebisha muundo wa biashara na mazoea ili kuendeleza malengo ya maendeleo endelevu, kuongoza njia ya kufikia fursa za kiuchumi kwa wanawake, na kufikia lengo la uhakika wa chakula duniani .  Hivyo amesisitiza  kwamba “Sasakuliko wakati mwingine wowote, ni wakati wa kutengeneza njia za ushirikiano katika dunia yetu lililogawanyika kwani dunia haiwezi kusubiri." 
More Episodes
Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ulifunga pazia hivi majuzi jijini New York Marekani ukipigia chepuo uwekezaji kwa wanawake na wasichana, na leo tunabisha hodi nchini Kenya wasichana waliokumbwa na ujauzito utotoni na kukatishwa ndoto za kuendelea na masomo au kupata...
Published 03/28/24
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “UDENDA”.
Published 03/28/24