20 JANUARI 2023
Listen now
Description
Hii leo jarida linaangazia mapigano Soledar Mashariki mwa Donetsk Oblast nchini Ukraine, na habari kuhusu afya kanda ya ulaya. Makala tunakwenda nchini Somalia na mashinani DR Congo. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limesema kwa mara ya kwanza misaada ya mashirika ya Umoja wa Mataifa imefanikiwa kuwasili katika eneo linalodhibitiwa na serikali karibu na Soledar Mashariki mwa Donetsk Oblast nchini Ukraine.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kanda ya ulaya tangu kuanza kwa msimu wa baridi kali katikati ya mwezi Novemba mwaka 2022 wamebaini kuongezeka kwa wagonjwa wanaolazwa kutokana na magonjwa ya homa ya mafua makali au flu, matatizo ya kupumua na COVID-19. Walio hatarini zaidi kupata maambukizi ya magonjwa hayo ni wahudumu wa afya pamoja na wazee, ndio maana wanaendesha kampeni ya kutoa chanjo..Makala tnaangazia kazi za WHO na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa likiwemo la uhamiaji, IOM na wadau wengine wakishirikiana kuwasaidia watu waliko katika hatari zaidi kwenye maeneo mbalimbali ya somalia wakiwemo waliofurushwa katika maeneo ya viunga vya mji wa Baidoa.Na katika mashinani tunakwenda jimboni Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako watoto wanafurahia kuwa wasafi shuleni kutokana na huduma za kujisafi zilizofanikishwa na UNICEF. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
More Episodes
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhiri; na  hadhiri.”
Published 04/18/24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina amabyo hivi karibuni tulizungumza na Peter Mmbando kutoka Tanzania akifafanua nini wanafanya ili kuimarisha matumizi endelevu ya teknolojia ya kidijitali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi na tofauti ya maneno “Adhiri; na ...
Published 04/18/24