Mabadiliko chanya darasani nchini Rwanda kupatikana kufuatia mtandao wa intaneti na ubunifu wa mwalimu.
Listen now
Description
Kuunganisha kila shule kwenye mtandao wa intaneti ndio msingi wa GIGA, mradi unaotekelezwa kwa pamoja na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia watoto UNICEF na la mawasiliano, ITU, yakitekeleza maono ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, mathalani Ajenda ya Pamoja.  Kupitia GIGA pengo la kidijitali linapungua; walimu wanafundisha kwa urahisi, wanafunzi nao wanakuwa wanapata taarifa kwa urahisi na za kisasa. Hata wakati wa COVID-19 GIGA ilikuwa mkombozi ukichanganya na ubunifu pia wa walimu. Lakini ni wapi hilo limetokea? Si kwingine bali Rwanda ambako ufungaji wa intaneti kwenye shule, pamoja na mgao wa vifaa kama vile kompyuta na projekta, au kifaa cha kuelekeza taarifa za kompyuta kwenye ubao, vimeleta mabadiliko kama inavyodhihirika kwenye makala hii kutoka UNICEF na kusimuliwa na Assumpta Massoi. 
More Episodes
Katika harakati za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kuna wakati jamii ambazo bado zinaishi kiasili zimekuwa zikilaumiwa kwamba zinachangia kuharibu mazingira kutokana na wao kuishi katika mazingira fulani; mathalani misitu na mbuga jambo ambalo linakanushwa na jamii hizo wakidai kwamba...
Published 04/15/24
Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani, Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili limeanza rasmi na litadumu kwa muda wa wiki mbili likiwaleta pamoja zaidi ya washiriki 2000 wa jamii za asili kutoka kila pembe ya dunia kujadili masuala...
Published 04/15/24