23 Januari 2023
Listen now
Description
Hii leo jarida linaangazia afya likikuletewa ripoti kuhusu ugonjwa wa moyo na WHO na, na pia tuanakupeleka nchini Madagascar kuangazia miradi mbalimbali. Makala na mashinani tunakwenda nchini Rwanda, kulikoni? Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa leo Jumatatu Januari 23, 2023 imebainisha kuwa watu bilioni tano duniani hawajalindwa dhidi ya viambato hatari vya mafuta vilivyoko katika bidhaa za vyakula vinazozalishwa viwandani na hivyo kuongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kifo.kupitia mradi wa mabadiliko ya haraka vijijini (RRT) shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP na wadau wake wameanzisha kituo maalum cha paneli za sola ambacho ni chanzo kikuu na endelevu cha maji na teknolojia ya mawasiliano ICT katika maeneo ya vijijini nchini Madagascar, hatua inayoruhusu upatikanaji wa huduma muhimu kama vile nishati, maji na mitandao ya kijamii kwa wakazi wa jamii hizo na kwa njia inayojali mazingira.Makala tunakwenda nchini Rwanda kuangalia ni vipi mpango wa mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa umeleta mabadiliko madarasani nchini humo.Na katika mashinani tutasalia huko huko nchini Rwanda kumsikia Murekatete Agnes, mtafiti wa kisayansi na mataalam wa maabara  katika maabara ya inayohusika na vyanzo, tiba na kuzuia magonjwa yanayohusiana na damu au Immunohematology. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
More Episodes
Wiki ya kimataifa ya chanjo ikifungua pazia, nchini Tanzania wahudumu wa afya kama Prisca Mkungwa wanajitoa kwa kadri ya uwezo wao kuhakikisha huduma za chanjo zinafikia walengwa wote hata wale walioko maeneo ya mbali. Mathalani huko wilayani Chunya, mkoani Mbeya, kusini magharibi mwa taifa hilo...
Published 04/24/24
Leo ni siku ya kwanza ya siku saba za Wiki ya Chanjo Duniani. (Taarifa ya Anold Kayanda) Wiki ya Chanjo Duniani ambayo huadhimishwa katika kila wiki ya mwisho ya mwezi Aprili, inalenga kuangazia hatua za pamoja zinazohitajika na kuhimiza matumizi ya chanjo kuwalinda watu wa rika zote duniani...
Published 04/24/24