24 JANUARI 2023
Listen now
Description
Ni Jumanne ya tarehe 24 mwezi Januari mwaka 2023 ambapo leo tunakwenda nchini Tanzania kuangalia juhudi zinavyofanyika kuhakikisha wanafunzi hususan wa vijijini wanakuwa na mazingira bora ya kuweza kujisomea  nyakati zote. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikimulika hali ya usalama DR Congo, ujumbe wa Katibu Mkuu ya siku hii ya elimu duniani na ripoti ya usafirishaji haramu wa binadamu. Katika mashinani tunakupeleka nchini Kenya. Hali ya usalama inazidi kuwa mbaya huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hususa jimboni Ituri ambako vikundi vilivyojihami vimeendelea kuua rai ana katika wiki sita zilizopita zaidi ya raia 200 wameuawa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya elimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kwamba elimu ni haki ya msingi ya binadamu na hivyo kila mtu anastahili kuipata. Kupitia ujumbe wake wa siku hii inayoadhimishwa kila mwaka Januari 24 Antonio Guterres amesema “Ni msingi wa jamii, uchumi, na uwezo wa kila mtu. Lakini bila uwekezaji wa kutosha, uwezo huu utaishia kwenye mzabibu".Na ripoti mpya iliyotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNDOC kuhusu usafirishaji haramu wa binadamu inaelezea hofu kwamba rasilimali za kuwaokoa waathirika wa usafirishaji haramu zimeelekezwa kwenye janga la COVID-19.Na leo katika mashinani tutakwenda Turkana nchini Kenya kumsikia Gabriel Ekaale, ambaye alianza kazi yake kama mwalimu wa shule ya upili nchini Kenya, lakini baada ya muda mfupi aligundua kwamba kazi yake inaweza kuwa na manufaa kwa jamii nzima, na sasa anafanya kazi na jamii zilizoathiriwa na ukame.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
More Episodes
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhiri; na  hadhiri.”
Published 04/18/24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina amabyo hivi karibuni tulizungumza na Peter Mmbando kutoka Tanzania akifafanua nini wanafanya ili kuimarisha matumizi endelevu ya teknolojia ya kidijitali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi na tofauti ya maneno “Adhiri; na ...
Published 04/18/24