25 JANUARI 2023
Listen now
Description
Hii Leo jaridani tunaangazia mkutano nchini Niger kuhusu kanda ya Ziwa Chad, na habari njema kwa wakulima wa vitunguu nchini Sierra Leone. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Uganda, kulikoni? Mkutano wa 3 wa Ngazi ya Juu kuhusu Kanda ya Ziwa Chad umehitimishwa leo kwa kuthibitishwa ahadi kutoka kwa nchi za Bonde la Ziwa Chad na wadau kwa mwitikio ulioratibiwa, wa kikanda na ulio endelevu.Vitunguu kuoza na kukosekana kwa kipato ulikuwa ni uhalisia kwa wakulima wa vitunguu kwenye mji wa Kabala nchini Sierra Leone wakati janga la COVID-19 lilipoibuka mapema mwaka 2020. Hali ilikuwa tete lakini kilio cha wakulima hao kilisikika na mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD ukaingilia kati. Nini kilifaniyika? Assumpta Massoi anafafanua kwenye ripoti hii iliyoandaliwa na IFAD.Katika makala nakuunganisha na Thelma Mwadzaya mwandishi wetu wa Nairobi Kenya akimulika harakati za Shirika la Umoja wa mataifa la Afya duniani, WHO kwa ushirikiano na serikali ya Kenya za kusambaza chakula tiba cha dharura cha msaada mahsusi kwa watoto walio na utapia mlo sugu.Na katika mashinani tunakwenda nchini Uganda kukutanana msichana muelimishaji rika ambapo anatumia nyimbo kuelezea wajibu wa wazazi na walezi wote kuachana na ndoa za utotoni kwa watoto wao wa kike na badala yake wapatiwe fursa ya masomo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda karibu!
More Episodes
Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ulifunga pazia hivi majuzi jijini New York Marekani ukipigia chepuo uwekezaji kwa wanawake na wasichana, na leo tunabisha hodi nchini Kenya wasichana waliokumbwa na ujauzito utotoni na kukatishwa ndoto za kuendelea na masomo au kupata...
Published 03/28/24
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “UDENDA”.
Published 03/28/24