Nchini Sierra Leone mashine ya kukausha vitunguu yarejesha neema kwa wakulima
Listen now
Description
Vitunguu kuoza na kukosekana kwa kipato ulikuwa ni uhalisia kwa wakulima wa vitunguu kwenye mji wa Kabala nchini Sierra Leone wakati janga la COVID-19 lilipoibuka mapema mwaka 2020. Hali ilikuwa tete lakini kilio cha wakulima hao kilisikika na mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD ukaingilia kati. Kabala, mji ulio kaskazini mwa Sierra Leone ni mzalishaji mkuu wa mazao mbali mbali kama vile mpunga, mihogo na vitunguu, lakini janga la COVID-19 lilipindua hali hiyo kama asemavyo Haja Thoa Conteh, mkulima wa eneo hilo, “COVID-19 ililipuka punde tu baada ya mavuno na hatukuweza kuuza kutokana na karantini. Ilibidi tuuze machungwa, mihogo, vitunguu, mchele kwa kiwango kidogo hapa kijijini ili tuweze kuishi. Lakini hali ilikuwa ngumu kabichi, karoti vilioza, hatukuweza kuuza kila kitu hivyo  tulipoteza kila kitu.”  Mmfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD ulitambua changamoto na kupitia kikundi cha wanawake wakulima hapa Kalaba, ambacho Bi. Conteh ni mwanachama, walipatiwa mradi wa kuchochea maendeleo kwa wakazi masikini vijijini.  Kupitia mradi huu walipatiwa pembejeo kama vile mbegu, mbolea, vifaa vya kilimo na mashine ya kukausha vitunguu ili waweze kurejea uzalishaji wa vitunguu kabla ya janga la COVID-19 na zaidi ya yote vitunguu viweze kukaa muda mrefu.  Wanakikundi walichanga fedha na kujenga jengo la kufunga mtambo na kukausha ili hatimaye wasubiri kuuza vitunguu wakati bei iko juu.  Mary Nabie Kamara, mwanakikundi anasema kuna mabadiliko makubwa kwa kuwa “kabla ya kupata mashine tuliuza vitunguu vyote kwa sababu hatukuwa na mahali pa kuhifadhi, hivyo vilioza. Lakini mwaka huu tumepata akiba ya dola 3,000 kwa sababu ya hii mashine mliyotupatia.”  Na kwa faida hii waliyopata, wanakikundi wanahifadhi kwa msimu ujao huku kiasi kidogo cha fedha wakisaidia wajane na yatima.  Sasa ni furaha! Na kwa Bi. Conteh, yeye anasema, “Hata kama mradi huu utaisha, tutaendeleza kilimo kwa sababu tumepata kianzio tulichohitaji, na stadi za kuendesha mashine tulizopatiwa ili tujikimu.” 
More Episodes
Hii leo jaridani utasikia kuhusu ushirikishwaji wa vijana katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Maendeleo UNDP. Pia utasikia muhtasari wa habari kuhusu wasaka hifadhi huko nchini Uingereza kuhamishiwa Rwanda, Makaburi ya halaiki huko Gaza na...
Published 04/23/24
Katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, afisa mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) anayehusika na masuala ya dharura na mnepo, Rein Paulsen ametahadharisha kuwa hatari ya kutokea baa la njaa nchini Sudan ni halisi na kwa hivyo wakati wa kuchukua hatua ni...
Published 04/22/24