Kenya: Mradi wa Teen Seed Africa warejesha matumaini ya elimu kwa wasichana waliopata mimba za utotoni
Listen now
Description
Umoja wa mataifa kwa ushirikiano na serikali ya Kenya ulizindua mwaka 2015 mradi wa kuwarejesha watoto shule walioacha kwa sababu moja au nyengine.  Kupitia mashirika mbalimbali kama Educate A Child, Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na lile la idadi ya watu duniani UNFPA ilizindua miradi ya pamoja ya kuwarejesha watoto shule.  Utafiti wa hivi karibuni  wa mashirika hayo umebainisha kuwa moja ya chanzo kikuu cha watoto wa kike kuacha shule ni mimba za utotoni na hususan watoto ambao wanaishi katika mitaa ya mabanda.   Maisha katika mitaa ya mabanda yana changamoto za kila aina ikiwmo usalama mdogo, msongamano, na uhaba wa huduma za kijamii ambavyo vyote vinachangia kuwapa changamoto kubwa wasichana.  Kwa mujibu wa UNFPA, kila siku, wasichana alfu 20 walio na umri ulio chini ya miaka 18 hujifungua. Hii ni sawa na watoto milioni 7.3 kwa mwaka kote duniani.  Miongoni mwa idadi hiyo asilimia kubwa ya wasichana hujikuta wakipata ujauzito katika umro mdogo na pindi msichana anapopata uja uzito basi maisha yake hubadilika kwa kiasi kikubwa.  Mimba za utotoni hupindua maisha ya mtoto wa kike kwani uwezekano wa kuacha shule au kurejea baada ya kujifungua kwa kiasi kikubwa ni mdogo sana.Mara nyingi chanzo cha mimba za utotoni ni ukosefu wa elimu au kusoma shuleni, taarifa na hata huduma mujarab za afya.   Hali hiyo ndiyo iliyolisukuma shirika la kijamii la Teen Seed lililoko mtaa wa mabanda wa Kiambio kuzindua mradi wa kuwarejesha shule wasichana waliopata mimba utotoni. Zawadi Anthony ni mratibu wa mradi wa Teen Seed Africa na anaelezea kuwa,”Wanapokuja wasichana tunakagua na kubaini iwapo wanataka na wana uwezo wa kurejea shule.Kisha tunahakikisha kuwa wanapata kila wanachohitaji ima ni vifaa vya shule, mlezi wa watoto au mtoto,bidhaa za matumizi na vyote anavyohitaji kukamilisha masomo yake.Kwa kawaida tunamtafutia shule hapa hapa karibu mtaani tu.”anafafanua.  Kulingana na utafiti wa mwaka 2021 wa tathmini ya watoto wasioenda shule uliofanya na mradi wa OOSC wa Educate A Child unayoshirikiana na UNICEF, watoto wasioenda shule walio na umri wa kati ya miaka 6 hadi 13 ni milioni 1.13 na wanazurura mitaani.  Ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO mwaka jana kuhusu changamoto za elimu inasema changamoto na vikwazo vya janga la COVID 19 vimesababisha na vinaendelea kuwaathiri wazazi wengi hasa katika nchini zinazoendelea kukimu mahitaji ya familia zao. Hii imechangia kwa baadhi ya watoto wa kike kujikuta pabaya na kuingilia mambo yasiyofaa kupata mkate wa kila siku. Quinta Faith ni msimamizi wa kitengo cha wasichana katika shirika la Teen Seed Africa na anaelezea wanachokumbana nacho ni,”Wasichana huamua kuolewa mapema wakiwa na miaka 14 au 16 kwani wamekosa wa kumtegemea kutimiza mahitaji yao ya kila siku.Umasikini ndio unaowasukuma kuwaegemea wanaume ambao wamewaonyesha mapenzi.”anasimulia.  Kwa ushirikiano na shirika la kijamii la Educate a Child, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, linafanya kazi pamoja na serikali ya Kenya kuiongeza idadi ya watoto wanaorejea shuleni baada ya kuacha shule kwa sababu moja au nyingine.  Mimba za utotoni ni moja ya sababu kuu za watoto wa kike kuacha masomo. Na mimba hizo zinaweza kutokea katika mazingira mbalimbali ikiwemo kwa na kuaacha wakiwa wamechanganiyikiwa.   Hapo ndipo Sharon Adema mshauri nasaha katika shirika la Teen Seed Africa anawapokea na kuwashika mkono na kwanza,” Tunawapokea wakiwa hali mbaya na ni dhahiri wamedhulumiwa kwani baadhi wana alama mwilini.Wakiridhia tunawapa ushauri nasaha na pia kuwapeleka hospitali kwa matibabu.Baada ya hapo tunashirikiana na afisi ya watoto ya serikali watakaoamua iwapo anaweza kurejea kwenye mazingira aliyokuwa au asalie mikonini mwao.Dhamira ni kuwaondoa kwenye mazingira magumu na hatari,” anasisitiza.  Shirika la Umoja wa Mataifa la UNFPA, liko mstari wa mbele pia kuunga mkono…
More Episodes
Wiki ya kimataifa ya chanjo ikifungua pazia, nchini Tanzania wahudumu wa afya kama Prisca Mkungwa wanajitoa kwa kadri ya uwezo wao kuhakikisha huduma za chanjo zinafikia walengwa wote hata wale walioko maeneo ya mbali. Mathalani huko wilayani Chunya, mkoani Mbeya, kusini magharibi mwa taifa hilo...
Published 04/24/24
Leo ni siku ya kwanza ya siku saba za Wiki ya Chanjo Duniani. (Taarifa ya Anold Kayanda) Wiki ya Chanjo Duniani ambayo huadhimishwa katika kila wiki ya mwisho ya mwezi Aprili, inalenga kuangazia hatua za pamoja zinazohitajika na kuhimiza matumizi ya chanjo kuwalinda watu wa rika zote duniani...
Published 04/24/24