Elimu ya usuluhishi na haki kusaidia kufanikisha SDGs Morogoro, Tanzania
Listen now
Description
Lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu SDGs yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015 linasisitiza amani, haki na taasisi thabiti. Uvunjivu wa amani utokanao na migogoro kwenye jamii ni moja ya maeneo yanayomuikwa ili kuhakikisha amani inakuweko na hivyo kuwezesha kufikia SDGs mwaka 2030. Nchini Tanzania, wiki ya sheria imefungua pazia na Mahakama Kuu inatimiza wajibu wake kusaidia nchi kufanikisha SDGs. Mathalani mkoani Morogoro, Mashariki mwa taifa hilo, Mahakama Kuu imesema sasa itasongesha zaidi elimu ya usuluhishi na haki kwa lengo la sio tu kujenga amani bali pia kuchochea uchumi. Je nini kinafanyika? Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM alikuwa shuhuda wetu na ameandaa makala hii, 
More Episodes
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhiri; na  hadhiri.”
Published 04/18/24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina amabyo hivi karibuni tulizungumza na Peter Mmbando kutoka Tanzania akifafanua nini wanafanya ili kuimarisha matumizi endelevu ya teknolojia ya kidijitali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi na tofauti ya maneno “Adhiri; na ...
Published 04/18/24