Siku hii ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji ina maana kubwa: Robi Samuel - Tanzania
Listen now
Description
Pamoja na kwamba juhudi zinaendelea duniani kote kutokomeza mila iliyopitwa na wakati ya ukeketaji, takwimu za Umoja wa Mataifa bado zinaonesha kuwa takribani watoto wa kike milioni 4.2 duniani wako hatarini kukeketwa mwaka huu wa 2023 pekee. Hata hivyo ni harakati za wadau mbalimbali kushiriki katika kutokomeza mila hii iliyopitwa na wakati ndizo zinategemewa kuhakikisha kuwa watoto hawa hawakumbani na madhila hayo. Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji, Robi Samuel Mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania lenye makao yake makuu Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara pamoja na mambo mengine likipambana dhidi ya mila iliyopitwa na wakati ya ukeketaji, yeye mwenyewe akiwa mmoja wa manusura wa tendo hilo la kikatili anaeleza siku hii ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji ina maana gani kwake
More Episodes
Hii leo jaridani utasikia kuhusu ushirikishwaji wa vijana katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Maendeleo UNDP. Pia utasikia muhtasari wa habari kuhusu wasaka hifadhi huko nchini Uingereza kuhamishiwa Rwanda, Makaburi ya halaiki huko Gaza na...
Published 04/23/24
Katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, afisa mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) anayehusika na masuala ya dharura na mnepo, Rein Paulsen ametahadharisha kuwa hatari ya kutokea baa la njaa nchini Sudan ni halisi na kwa hivyo wakati wa kuchukua hatua ni...
Published 04/22/24