07 FEBRUARI 2023
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tunakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako mapigano yanayoendelea yanatenganisha watoto na familia zao na sasa hatua zinachukuliwa kuunganisha watoto na familia zao. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zinazohusiana na janga la tetemeko la ardhi katika mashariki ya kati na pia hali ya usalama nchini Somalia. Mashinani tutasalia huho huko nchini Somalia. Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa nchini Syria Paulo Pinheiro amesema yeye na makamishina wengine wa Umoja wa Mataifa pamoja na timu za misaada wanatoa pole kwa maswahibu yaliyowakumba wananchi wa nchi hiyo na kutoa ombi maalum la pande zote zinazo zozana nchini Syria kuweka silaha chini ili kuwaruhusu wahudumu wa misaada ya kibinadamu na waokoaji kuweza kuwafikia wenye uhitaji bila ya kuwa na wasiwasi wa kushambuliwa.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO linalohusika pia na usimamizi wa maeneo ya kuhistoria limesema limeanza uchunguzi wa awali kuangalia maeneo ya kuhistoria yaliyoathiriwa na matetemeko. Na tumalizie habari kwa ufupi kutoka Geneva nchini Uswisi ambapo kufuatia mauaji yaliyotokea baada ya mapigano makali kutokea kuanzia tarehe 5 mwezi huu wa Februari nchini Somalia kati ya vikosi vya usalama na wanajamii wa ukoo wa Laas Canood, Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk ametoa wito kwa mamlaka ya Somalia kuhakikisha uchunguzi huru unafanyika bila upendeleo.Na katika mashinani tutaelekea Doolow nchini Somalia kusikia ujumbe wa Dkt. Natalia Kanem, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
More Episodes
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhiri; na  hadhiri.”
Published 04/18/24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina amabyo hivi karibuni tulizungumza na Peter Mmbando kutoka Tanzania akifafanua nini wanafanya ili kuimarisha matumizi endelevu ya teknolojia ya kidijitali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi na tofauti ya maneno “Adhiri; na ...
Published 04/18/24