Description
Hii leo jaridani tunaangazi ufadhili kwa wakulima huku mkutano wa COP29 ukiendelea Baku, na madhara ya mafuriko kwa wakulima nchini Sudana Kusini tukimulika jinsi Umoja wa Mataifa wanavyohaha kuwasaidia. Makala inatupeleka nchini DRC na mashinani tunasalia huko huko Sudan Kusini, kulikoni?
Kuongeza kiwango cha fedha kwenye ufadhili wa miradi ya kukabili na kuhimili tabianchi nchi ikiwa ni moja ya masuala muhimu yanayojadiliwa katika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 huko Baku, Azerbaijan, leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema bila kupunguza kwa kiasi kikubwa hewa chafuzi, na kuimarisha miradi ya kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi, kila uchumi duniani utakumbwa na madhara makubwa.Huko Maban, jimboni Upper Nile, kaskazini mashariki mwa Sudan Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linajenga vifaa vya kuhifadhi maji pamoja na makinga maji ili kuepusha mashamba dhidi ya mafuriko ya msimu yanayokumba eneo hilo mara kwa mara, eneo ambalo ardhi yake ina rutuba kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara.Katika Makala George Musubao, mwandishi wetu huko Jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akimulika mkutano ulioandaliwa na watendaji wa Umoja wa Mataifa ya eneo hilo kuangalia jinsi ya kukabiliana na habari potofu na za uongo.Na mashinani tutakuwa Sudan Kusini, ambako shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP linasaidia jamii zilizoathiriwa na mafuriko kupata suluhisho la kudumu.Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania umewajumuisha watoto kwenye harakati za kukabiliana na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Huko Baku nchini Azerbaijan kunakotamatika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya...
Published 11/22/24
Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili...
Published 11/22/24