15 NOVEMBA 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunaangazia suala muhimu wa mabadiliko ya tabianchi tukijikita kataika mkutano wa COP29 huko Baku Azerbaijan kuwasikia wanaharakati wa mazingira kutoka nchi mbalimbali. Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 u unaofanyika Baku Azerbaijan, leo umejikita na ongezeko la gesi chafuzi ya methane ambayo kwa kiasi kikubwa inatokana na shughuli za binadamu ikiwemo ufugaji wa ng’ombe, na sasa nini kifanyike ili kuidhibiti.Tunasalia huko huko Baku, Azerbaijan. Wito umetolewa kwa wanawake ambao ni waathirika wakubwa wa janga la mabadiliko ya tabianchi wasipewe kisogo katika harakati za kuhimili na kukabili madhara ya janga hilo.Katika makala Bosco Cosmas anatupeleka Amerika ya Kusini kusikia harakati za mwanamke wa jamii ya asili za kulinda eneo lao.Mashinani leo Fathimath, kijana kutoka Maldives anatoa kauli kwa ajili ya hatua za dharura kupambana na mabadiliko ya tabianchi katika mkutano wa COP29.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
More Episodes
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania umewajumuisha watoto kwenye harakati za kukabiliana na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Huko Baku nchini Azerbaijan kunakotamatika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya...
Published 11/22/24
Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili...
Published 11/22/24