Let's keep it real, we need each other (Part 1)
Listen now
Description
Ni karne ya 21, na mapinduzi mengi sana ya kimaendeleo yametokea duniani na yanaendelea kutokea. Na tunajua kwamba ili tuweze kuendelea kuwa bora kama jamii na kamą wanadamu basi hatuna budi kuyakumbatia mapinduzi yenye tija na yenye kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu. Moja ya mapinduzi ambayo kama binadamu tumechelewa sana kuanza kuyapambania kwa nguvu zote ni mapinduzi juu ya usawa wa kijinsia. Hili ni jambo jema na lenye msingi wenye kuleta heri kwa jamii nzima. Lakini, ili mapinduzi haya yafanikiwe na yaweze kufikiwa malengo yanayopaswa kufikiwa basi ni lazima jinsia zote mbili ziweze kushiriki kikamilifu katika mchakato huu. Swali ambalo tunajiuliza leo kwa undani, ni je wanaume wanashiriki kikamilifu katika mapambano na mchakato wa kuleta haki sawa kwa jamii yetu? Kama wanashiriki, nini imekua mchango wao? Na kama hawashiriki, ni kitu gani kinazuia ushiriki wao kikamilifu? Hofu ya wanaume ni nini kwenye hili? Chimbuko la hofu hiyo ni nini? Na ni vipi tunaweza kumshirikisha mwanaume huyu kikamilifu kwenye hii safari? Sababu kiukweli kabisa, wanaume na wanawake wote wanahitajiana kwa ustawi bora wa jamii Rolland Malaba A.K.A Madenge amejadili swala hili kwa undani na kujaribu kuchanganua baadhi ya mambo akishirikiana na Michael Baruti pamoja na Nadia Ahmed. Karibu usikilize Sehemu ya kwanza ya maongezi haya
More Episodes
This is the Allan Lucky’s story of how he went against all odds to become the man he is today. Born in Songea, to a christian Family, Allan describes his early life as being constrained in the triangle of three main things, church, school and home. From an early age it seemed that this is how...
Published 04/02/24
Published 04/02/24
In this captivating episode, join us as we sit down with Hisia, a remarkable individual whose journey from humble beginnings in Arusha to musical acclaim and entrepreneurial success in Dar es Salaam is nothing short of inspiring. From immersing himself in the world of sales and marketing at...
Published 03/19/24