Parenting from a distance
Listen now
Description
Jambo la kutafuta kwa ajili ya kuangalia na kuhudumia familia yako ni jambo ambalo halikwepeki kwa mwanaume, tena ikiwa ni mwanaume anaewajibika katika majukumu yake. Lakini, kwenye kutafuta wanaume wengi sana wamejikuta ikiwabidi kwenda kuishi mbali na familia zoo ili waweze kuzihudumia na pia waweze kutimiza ndoto walizonazo juu ya familia zao. Kuishi mbali na familia kunakuja na changamoto nyingi sana ambazo labda jamii haizitambui. Wanaume wengi wanateseka na namna ya kulea watoto wao, lakini pia hata namna ya kuboresha mahusiano na wenzi wao huku wakikabiliana na umbali uliopo kati yao. Philip Changala alihamia Dar es Salaam kutoka Dodoma mwaka 2016, akaacha familia yake Dodoma yenye mtoto mdogo kabisa. Leo hii ameamua kuzungumza na sisi namna maisha ya kuwa mbali na familia, hususani familia changa inavyoweza kuwa na changamoto nyingi sana kwa mwanaume, na namna ambavyo inaweza kuwa chanzo kikubwa cha changamoto ya afya ya akili kwa mwanaume. Nadia anaelezea namna ambavyo mwanaume anaweza akapambana na hali hiyo, lakini pia ni hatua zipi za kuchukua ili kuhakikisha nafasi yako kama baba na kama mume bado inabaki hata kama maisha yamekupeleka mbali na familiÄ… yako
More Episodes
This one is for the books. Our episode with Walter Bgoya, a senior citizen and longtime publisher in Tanzania, is all about intergenerational conversations. Walter dives into this episode and shares his insights as a man on parenting, business, relationships, his values as a man but also,...
Published 10/28/22
Published 10/28/22
Linapokuja swala la ndoa na mafanikio ya ndoa watu wengi huwa na mitazamo tofauti. Wapo wanaosema ndoa ni ngumu na si rahisi kufanikiwa kwenye ndoa, na wapo wanaosema ndoa ni ngazi ya mafanikio pale wanandoa wanapokubaliana kwenye hilo. Leo hii, sisi tunajiuliza, ni nini nafasi ya mwanaume...
Published 10/13/22