SE7EP08 - SALAMA NA SAMATTA | HEADMASTER
Listen now
Description
Kila kijana wa ki Tanzania ambae anaupenda na kuuthamini mpira wa miguu na ambaye angependa ndo iwe kazi ya maisha yake basi Mbwana Ally Samatta ndiye role model wake, hakuna doubt kwamba watakua na mapenzi na Cristiano Ronaldo au Leo Messi au Kylian Mbappe au Marcus Rashford ila yule ambaye amewaaminisha kwamba INAWEZEKANA ukacheza POPOTE hapa duniani na hasa kwenye ligi yetu pendwa ya Uingereza ni Samatta. Rafiki tu kutoka Mbagala rangi tatu ambaye kashacheza saaana ndondo na makombe ya mbuzi wakati anakua na mwisho wa siku akaenda kucheza kwa wazungu na bado anaendelea kutafuta rizki yake huko, hata kama sio ligi ile ambayo hata yeye mwenyewe angependa awepo ila BADO ni MWAMBA wetu. Samatta huyu huyu ndo ambaye alijitwika mpira kichwani na kuitika nyavuni mbele ya beki ambae anaaminika kuwa BORA kwa misimu hii miwili mitatu ndani ya Virgil van Dijk. Hata wakati naandika hii bado mwili unanisisimka kwa wazo tu kwamba nililishuhudia lile, pata picha kwa mtoto ambaye ana ndoto hizo. Lile goli lilimfanyia NINI kwenye ndoto zake. KRC Genk walipoteza mchezo ule wa ugenini wa kombe la mabingwa wa Ulaya kwa magoli 2-1 ila kwenye mitaa yote ya mikoa ya Tanzania ile mechi ilikua ya USHINDI. Mbwana ametokea kwenye familia ya kawaida sana sana, wazazi wake wote kama kumbukumbu yangu itakua 100 basi walikua polisi, najua kwa hakika Baba yake alikua Polisi kwa asilimia 100. Kwa marehemu Bi Mkubwa wake ndo sina hakika sana ila kwa hakika jibu limo kwenye haya maongezi yetu. Anakumbuka jinsi ambavyo Mzee wake alikua anasisitiza kwenye suala la elimu na heshima, kama mtoto wa mwisho kwenye familia hiyo, Mbwana aliupenda sana mpira, zile za kujiiba na kwenda kucheza mechi za mbali alishafanya sana na matunda ndo haya ya leo. Nadhani ilifika kipindi Mzee mwenyewe aliona basi sawa, twende huko utakako. Familia yao yote ni wapenzi wa mpira na Kaka yake Mouhamed bado anacheza hapa hapa Tanzania. Sasa akiwa kama kioo kikubwa sana kwenye jamii hii Samatta anazungumzia presha ambayo hupewa hasa pale anapoitwa kwenye timu ya Taifa, jinsi maneno mengi ya kashfa yanaporushwa kwake kutoka kwa wananchi na anakumbuka pia wakati bado anacheza T.P Mazembe kuna kipindi kocha aliacha kumuita yeye na Rafiki yake Thomas Ulimwenguna ilisemekana kama pengine hakuna na interest na team au hakua anatoa 100. Pengine kipindi hicho aliumia zaidi maana hiyo haikua jambo zuri kwake. Mbwana anazungumza na mimi kuhusu urafiki wake na Ulimwengu na maisha ambayo walikua wanaishi pamoja wakati wako DRC, anakumbuka jinsi walivyokua wanapanga kufanikiwa pamoja na mipango yao endelevu kwenye career yao. Ulimwengu nae ana siku yake kwenye kiti chetu In Shaa Allah maana nae ana mengi ya kutuelezea. Majeraha ya mara kwa mara bila ya shaka yalisababisha kwa kiasi kikubwa ndoto zake za kucheza Ulaya kutochukua hatua ya juu kama ambavyo angependa, ila mimi naamini hayo yote maisha tu, kila kitu kilikua tayari kimesha andikwa. Samatta ni Baba ambaye watoto wake wanasoma hapa hapa nyumbani, nilimuuliza kama watoto wake wanajua yeye ni nani na akanipa story ndogo ya yeye kung’amua kama wanafahamu fika Baba yao ni nani. Mwenzangu humu kuna mengi sana ambayo yatakufaa na kwa nafasi ya kipekee ningependa kumshukuru Captain wa Taifa kwa kuchukua time kwenye ratiba yake ambayo ilikua imebana kweli kweli ili tu aje kutubarikia meza yetu kwa uwepo wake. Yangu matumaini uta enjoy sana. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
More Episodes
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa...
Published 03/02/23
Published 03/02/23
Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan...
Published 02/23/23