Ep. 53 - Salama Na NANDY | MNOGESHAJI
Listen now
Description
Huyu si moja ya marafiki zangu, as in si Mtu amable nafahamiana naye sana, ambaye nishawahi kukaa naye muda mrefu na kupiga story, au kusafiri naye au kuwa studio wakati anafanya mambo yake au namjua mzazi wake au mtu wake wa karibu kwenye familia yake ila nawajua watu ambao wanamfahamu kwa ukaribu na watu hao ndo ambao walinipa mimi mawazo ya kutaka kumfahamu vizuri binti huyu hodari wa ki Tanzania bila ya hata ya wao kujua. Baadhi ya Dada zangu walifahamiana naye kwenye kipindi cha msiba wa Marehemu Ruge Mutahaba, kipindi hiko kilikua cha masikitiko kwao na kwake pia. Nandy alikua na ukaribu mwingi na Ruge, alishawahi kumtembelea hospitali mara kadhaa na pia alikua na mawasiliano ya moja kwa moja na watu wa karibu wa familia kipindi kile ambacho Ruge alikua hana tena mawasiliano naye moja kwa moja. Siku ambayo Ruge alitangulia muelle ya haki, muda si mrefu kabla ya hilo halijatokea Nandy ananiambia alizungumza na nesi wa zamu siku hiyo na pia alimuekea simu kwa ukaribu na alimsikia akiwa anapumua. Wapi alikua wakati anapata habari hii iko kwenye maongezi yetu haya, humu pia utaelewa connection ambayo sisi binadamu tunayo na watu ambao tunawapenda na wanao wanatupenda. Najua siku hazigandi kama ambavyo Lady Jd alishawahi kuimba na ndo  nikawaza, hivi ushawahi kuwaza Nandy amekua kiasi gani toka msiba wa Ruge utokee? Unakumbuka baadhi ya maneno yalosemwa juu ya career yake baada ya msiba ule? Tunafahamu kwamba alipoteza rafiki, mentor, baba na kama tochi yake? Mimi huwaza haya sana, na hilo la yeye kujidhatiti na kukaza mwendo ndo ambalo lilifanya mimi binafsi niseme you know what, it’s time. Nandy ni MPAMBANAJI, anaupenda muziki na kama mtu mwengine yoyote mwenye jitihada basi Mungu humfungulia milango ya Kheri. Kaniambia humu kwenye mangezi yetu kwamba safari yake ya kwanza kwenda nchini Nigeria kwenye mashindano ya kuimba alimuambia Mama yake wakati yumo ndani ya ndege, alipomaliza hutuba yake fupi alizima simu na wheels up, to Lagos ambako alihakikisha anapigana mpaka fainali na kumaliza nafasi ya tatu. Si kitu kidogo kwa binti ambaye aliamua kuweka shule pembeni ili atimize ndoto yake, ndoto ambayo hata Mama yake mzazi hakua na taarifa nayo. Siku zinakwenda, maisha yanasonga na yeye ameendelea kukimbiza ndoto yake na mpaka tunaenda mitamboni, Nandy ni mmoja wa wasanii wa kike wakubwa sana hapa nyumbani na barani Afrika na hata Ulaya na Marekani na ukitizama vizuri utajua kwamba huu ni mwanzo tu wa mazuri ambayo yatatokea katika maisha yake. Mimi na yeye tulizungumzia mahusiano hayo pamoja na kukimbiza ndoto zetu. Tuliongelea Bill Nas na kiwanda cha muziki wa Bongo Flava. Tuliongelea muziki wake na collabo ambazo amewahi kufanya. Hapo hapo nilitaka kujua pia yeye ni mtu wa aina gani na ni vitu gani vinamsukuma kutaka atake zaidi na sehemu ambayo anajiona huko mbeleni In Shaa Allah. Yangu matumaini kama kawaida ni kwamba utajifunza mawili matatu ambayo yatakusaidia kupambana na mitihani ya maisha kwasababu tu umejifunza kutokana na sehemu wenzetu hupitia kwenye maisha yao. Tafadhali Enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
More Episodes
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa...
Published 03/02/23
Published 03/02/23
Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan...
Published 02/23/23