4 episodes

BW MUNGU NASHANGAA KABISA.

How Great Thou Art.

Tenzi 114.

                                     Na, Stuart Keene Hine 1899 - 1989.

Bw. MUNGU Nashangaa Kabisa! Umechaguliwa na wapenzi wa nyimbo za sifa huko Great Britain, kuwa utenzi wa Rohoni unaotumika kwenye hafla nyingi nchini humo.

Nchini Marekani “Bw. MUNGU Nashangaa Kabisa!” ulirekodiwa na Elvis Presley na wasanii wengine wengi. Ulikuja kuwa sauti kuu [main vocal] iliyotumika kwenye matangazo ya kipindi cha kila wiki cha Billy Graham’s Hour of Decision [Saa ya uamuzi ya Billy Graham] na ulijipatia tuzo mbili za Grammy.

Stuart aliguswa kuandika utenzi wake ndani ya miaka 14 na kwa mara ya kwanza kuuingiza katika jarida lake la Injili lililojulikana kwa jina la Grace and Peace [Neema na Amani] la tarehe 15 Aprili 1949. Mguso wake kwa wimbo huu ulitokana na uzoefu wake mwenyewe alioupitia katika milima ya Carpathian na kusikiliza kutoka utenzi wa Ivan Prokhanoff Mwana-utenzi wa Kirusi aliyeghani wimbo wake wa Mungu mwenye nguvu [Mighty God] ambao aliuegemeza kwenye shairi la Carl Boberg la “O Store Gud”.

Stuart Keene Hine alizaliwa Magharibi mwa London mnamo tarehe 25 Julai 1899, kama mvurugano vile, karne mpya ilikaribia. Alikata shauri mwenyewe kwa ajili ya Kristo katika umri wa miaka 14 na muda mfupi baadaye alibatizwa. Katika umri wa miaka 18, Stuart aliitwa kwa ajili ya utumishi katika jeshi nchini Ufaransa. Hizi zilikuwa siku za utisho, lakini imani ya Mtumishi wa MUNGU Stuart ilibaki kuwa imara. Akirudi London disemba 1919, Stuart mwishowe alipata ajira kama karani katika kampuni ya kimataifa ya Kijapani ya Mitsubishi.

Yapata mnamo 20 Juni 1923, katika Kanisa la Manor Park Baptist Church, Mtumishi wa MUNGU Stuart alimuoa Mercy Salmon na ndani ya mwezi mmoja tu wa ndoa yao waliamua kwenda Poland kuanza kipindi cha utumishi katika Ulaya Mashariki ambao ulikuwa ukamilike kwa zaidi ya miaka 16. Mnamo mwezi Juni 1934 Mtumishi Stuart alianza safari ya umissioni ya maili 300 kwa baiskeli kuwafikia watu wa viunga vya Carpathian Mountains, ebu fikiria ni muda gani ingemgharimu. Ni safari hii ndiyo ilizaa utenzi wake wa “Bw. MUNGU Nashangaa Kabisa!” Akiwa njiani aliona jinsi ya mandhari maridadi ya uumbaji wa MUNGU katika ile milima, galaksi za angani, viumbe vilivyomo katika ile milima, uvumi wa mito, milio ya ndege wa angani na wanyama, uvumi wa miti wakati upepo unapovuma “Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo, na miti yote ya kondeni itapiga makofi Isa.55:12”, akavutiwa Rohoni sana na ukuu, uweza, mamlaka na nguvu za MUNGU. 

Hata wewe na mimi ni kazi ya mikono toshelevu ya MUNGU na ametuumba kwa jinsi ya ajabu pia, wewe na mimi tuna hazina ya kipekee ambayo haikuwahi kuwepo duniani na huenda isiwepo tena, mshukuru MUNGU kwa jinsi ulivyo kwa maana kuna mtu akikuona anakutamani jinsi ulivyo na kusema moyoni mwake hakika huyu amebarikiwa, hakika MUNGU unanishangaza sana kwa jinsi ulivyomuumba huyu ninayemuona hivi sasa!. Kuna watu wengine hawaoni utu wako wa nje lakini wanaona utu wako wa ndani na kuutamani sana jinsi ulivyo. Ukitaka pia kutafakari ukuu wa MUNGU ebu fikiria zile galaksi [nyota za angani] ambazo hadi sasa kwa mujibu wa wanajimu zimegunduliwa zaidi ya milioni 300 [ugunduzi unaendelea] ambazo ni kubwa na nzito kuliko sayari ya dunia hii tunayoishi na zinaelea tu huko anga za juu [space] bila ya nguzo iliyozishika na ajabu zaidi ni pale zinapojizungusha na kulizunguka jua pasina kukosea njia zao [bila kugongana] hata kidogo tangu uumbwaji wao, huku tukiambiwa kuwa kwa ukubwa na uzito wao, moja tu ikidondokea dunia hii tunayoishi basi itasambaratishwa kabisa na mahala pake pasijulikane asilani! Lakini ebu ona jinsi ambavyo zinatii amri na uweza wa NENO la MUNGU iliyoziweka huko. Kwa tafakari hii kwa nini tusimshangae MUNGU kabisa kama ambavyo Mtumishi Stuart alivyomshangaa. 

SHUHUDA ZA TENZI NA EMMANUEL SHEDO Mc foma foma

    • Arts

    Kurunzi la Tenzi Na Emmanuel Shedo

    Kurunzi la Tenzi Na Emmanuel Shedo

    NASIKIA KUITWA.

    I Hear Thy Welcome Voice.

    Na, Lewis Hartsough 1828 - 1919.

    Lewis Hartsough alizaliwa Agosti 31, 1828, Ithaca, New York Marekani na alihitimu masomo yake huko Cazenovia Seminary mwaka 1852. Aliwekwa wakfu kuwa Mtumishi wa ki-methodist [Methodist Minister] mwaka 1853, na alijiunga na Oneida Conference ya New York Marekani. Yapata mwaka 1868, alihamia magharibi mwa nchi kwa sababu za kiafya, ambapo alikujakuwa mwangalizi mkuu wa the Utah Mission, baadaye mzee mwangalizi wa the Wyoming District. Katika kipindi hicho hicho alitumika kama Mhariri wa muziki wa Joseph Hillman’s Revivalist. Mnamo mwaka 1871, Lewis Hartsough alisimikwa kuwa Pastor wa Methodist church huko Epworth, Iowa. Alihamia Northwest Iowa Conference mwaka 1874, na kustaafu mwaka 1895. Roho yake ilitwaliwa Mbinguni Januari 1, 1919 na mwili wake kuhifadhiwa huko Mount Vernon, Iowa Marekani. 

    “Nasikia Kuitwa” uliotungwa mwaka 1872 na mpaka sasa ambapo kitabu hiki kinakuijia umelihudumia Kanisa kwa miaka ipatayo 143, ni wimbo ambao wakati wowote uwao ule unapoimbwa basi kila muamini katika Kristo aliye hai, anapata msisimko unaoalika uwepo wa ajabu sana na kupelekea kuzama katika kumtafakari Kristo katika hali ya Rohoni zaidi. Wimbo huu ni kati ya nyimbo za Tenzi zinazopendeka sana miongoni mwa Wakristo wanaouchukulia utume mkuu wa YESU Kristo duniani kwa namna ya kipekee sana. 

    Asili na muktadha wa wimbo huu vinaegemea katika ukombozi wa msalaba na kuuhishwa kwa njia ya damu ya thamani ambapo dhambi/taka zinasafishwa na unyonge unabadilishwa na nguvu mpya ya upendo, imani na tumaini la Mbinguni. Ni wimbo ambao umemtangazia shetani waziwazi kushindwa kwake na mioyo yetu ya imani inashuhudiwa hivyo na kwamba zipo ahadi, haki na nguvu ndani ya wokovu wetu kama tukiamini.

    Ujumbe wa “Nasikia Kuitwa” wa Pastor Lewis, unadhihirisha kama vile alikuwa katika uhitaji [labda kutokana na afya yake na huduma yake] ambapo baada ya kuzama katika kuutafuta uso wa MUNGU akasikia sauti ikimwita apasogelee msalaba kwa ajili ya utakaso kwa njia ya damu ya YESU. 

    Mimi na wewe ni mara ngapi tuwapo katika utumishi wetu na labda katika hali ya kuhitaji tumetulia mbele za MUNGU kwa ajili ya kusikia sauti yake? Tunaweza kuleta hesabu zetu mezani kuthibitisha madai haya?

    • 7 min
    Ni salama Rohoni Mwangu

    Ni salama Rohoni Mwangu

    Maneno ya Wimbo yametungwa na Horratio gates Spaffod na Sauti tune ni Philip P. Bliss waimbaji ni kwaya ya Gospel Kijenge Arusha Tanzania East Africa

    • 6 min
    Semina ya wana ndoa Mwalimu T. Mzava

    Semina ya wana ndoa Mwalimu T. Mzava

    Semina inayoendea usharika wa Kijenge Arusha KANISA LA KIINJILI TANZANIA

    • 1 hr 6 min
    SHUHUDA ZA TENZI na Emmanuel Shedo

    SHUHUDA ZA TENZI na Emmanuel Shedo

    BW MUNGU NASHANGAA KABISA.

    How Great Thou Art.

    Tenzi 114.

                                         Na, Stuart Keene Hine 1899 - 1989.

    Bw. MUNGU Nashangaa Kabisa! Umechaguliwa na wapenzi wa nyimbo za sifa huko Great Britain, kuwa utenzi wa Rohoni unaotumika kwenye hafla nyingi nchini humo.

    Nchini Marekani “Bw. MUNGU Nashangaa Kabisa!” ulirekodiwa na Elvis Presley na wasanii wengine wengi. Ulikuja kuwa sauti kuu [main vocal] iliyotumika kwenye matangazo ya kipindi cha kila wiki cha Billy Graham’s Hour of Decision [Saa ya uamuzi ya Billy Graham] na ulijipatia tuzo mbili za Grammy.

    Stuart aliguswa kuandika utenzi wake ndani ya miaka 14 na kwa mara ya kwanza kuuingiza katika jarida lake la Injili lililojulikana kwa jina la Grace and Peace [Neema na Amani] la tarehe 15 Aprili 1949. Mguso wake kwa wimbo huu ulitokana na uzoefu wake mwenyewe alioupitia katika milima ya Carpathian na kusikiliza kutoka utenzi wa Ivan Prokhanoff Mwana-utenzi wa Kirusi aliyeghani wimbo wake wa Mungu mwenye nguvu [Mighty God] ambao aliuegemeza kwenye shairi la Carl Boberg la “O Store Gud”.

    Stuart Keene Hine alizaliwa Magharibi mwa London mnamo tarehe 25 Julai 1899, kama mvurugano vile, karne mpya ilikaribia. Alikata shauri mwenyewe kwa ajili ya Kristo katika umri wa miaka 14 na muda mfupi baadaye alibatizwa. Katika umri wa miaka 18, Stuart aliitwa kwa ajili ya utumishi katika jeshi nchini Ufaransa. Hizi zilikuwa siku za utisho, lakini imani ya Mtumishi wa MUNGU Stuart ilibaki kuwa imara. Akirudi London disemba 1919, Stuart mwishowe alipata ajira kama karani katika kampuni ya kimataifa ya Kijapani ya Mitsubishi.

    Yapata mnamo 20 Juni 1923, katika Kanisa la Manor Park Baptist Church, Mtumishi wa MUNGU Stuart alimuoa Mercy Salmon na ndani ya mwezi mmoja tu wa ndoa yao waliamua kwenda Poland kuanza kipindi cha utumishi katika Ulaya Mashariki ambao ulikuwa ukamilike kwa zaidi ya miaka 16. Mnamo mwezi Juni 1934 Mtumishi Stuart alianza safari ya umissioni ya maili 300 kwa baiskeli kuwafikia watu wa viunga vya Carpathian Mountains, ebu fikiria ni muda gani ingemgharimu. Ni safari hii ndiyo ilizaa utenzi wake wa “Bw. MUNGU Nashangaa Kabisa!” Akiwa njiani aliona jinsi ya mandhari maridadi ya uumbaji wa MUNGU katika ile milima, galaksi za angani, viumbe vilivyomo katika ile milima, uvumi wa mito, milio ya ndege wa angani na wanyama, uvumi wa miti wakati upepo unapovuma “Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo, na miti yote ya kondeni itapiga makofi Isa.55:12”, akavutiwa Rohoni sana na ukuu, uweza, mamlaka na nguvu za MUNGU. 

    Hata wewe na mimi ni kazi ya mikono toshelevu ya MUNGU na ametuumba kwa jinsi ya ajabu pia, wewe na mimi tuna hazina ya kipekee ambayo haikuwahi kuwepo duniani na huenda isiwepo tena, mshukuru MUNGU kwa jinsi ulivyo kwa maana kuna mtu akikuona anakutamani jinsi ulivyo na kusema moyoni mwake hakika huyu amebarikiwa, hakika MUNGU unanishangaza sana kwa jinsi ulivyomuumba huyu ninayemuona hivi sasa!. Kuna watu wengine hawaoni utu wako wa nje lakini wanaona utu wako wa ndani na kuutamani sana jinsi ulivyo. Ukitaka pia kutafakari ukuu wa MUNGU ebu fikiria zile galaksi [nyota za angani] ambazo hadi sasa kwa mujibu wa wanajimu zimegunduliwa zaidi ya milioni 300 [ugunduzi unaendelea] ambazo ni kubwa na nzito kuliko sayari ya dunia hii tunayoishi na zinaelea tu huko anga za juu [space] bila ya nguzo iliyozishika na ajabu zaidi ni pale zinapojizungusha na kulizunguka jua pasina kukosea njia zao [bila kugongana] hata kidogo tangu uumbwaji wao, huku tukiambiwa kuwa kwa ukubwa na uzito wao, moja tu ikidondokea dunia hii tunayoishi basi itasambaratishwa kabisa na mahala pake pasijulikane asilani! Lakini ebu ona jinsi ambavyo zinatii amri na uweza wa NENO la MUNGU iliyoziweka huko. Kwa tafakari hii kwa nini tusimshangae MUNGU kabisa kama ambavyo Mtumishi Stuart alivyomshangaa.

    • 4 min

Top Podcasts In Arts

Fresh Air
NPR
The Moth
The Moth
99% Invisible
Roman Mars
Add to Cart with Kulap Vilaysack & SuChin Pak
Lemonada Media
The Recipe with Kenji and Deb
Deb Perelman & J. Kenji López-Alt
Snap Judgment Presents: Spooked
Snap Judgment