Episodes
Join the conversation with Yesaya and Anderson to talk about Switching/Sticking to Programming Languages.
Published 08/10/23
Published 08/10/23
Kwenye episode hii nimeeleza kwa kina namna ya kuandika ujumbe wa kuomba msaada kwa mtu mwenye followers wengi. Yawezekana ni programmer au mtu mwenye uzoefu kwenye eneo fulani.
Published 01/30/23
Nimeandaa mjumuisho wa mambo niliyojifunza kwenye #DevFestNairobi na hamasa niliyopata na hivyo nimeona vyema niweze kukushirikisha wenzetu walipo ili nasi tupate kupiga hatua zaidi. Ndugu yangu, sikuwahi kujua event ya developers kuwa na wahudhuliaji zaidi ya 3000, vyombo kuletwa na kontena la 40 futi. Yaani nina mengi kukubadilisha mtazamo lakini nikaelewa ndio maana makampuni makubwa ya TEHAMA duniani yana ofisi Kenya. DevFestDar RSVP: http://zipa.me/devfestdar Be a Speaker:...
Published 11/16/22
Tunapoelekea kufungua vyuo, nimeona ni vyema kuwapa abc wanafunzi wa mwaka wa kwanza hasa katika kozi za TEHAMA. Nimeweka mambo matatu (3) muhimu ya kuzingatia, unaweza niachia maoni yako kule Twitter @yesayasoftware.
Published 10/14/22
Browser ni software application for retrieving, presenting and traversing information resources on the World Wide Web. Lakini pia inawezesha kucapture au kuinput taarifa ambayo inaweza kurudishwa kwa mfumo unaowasilisha, kisha kuhifadhiwa au kuchakatwa inapohitajika.
Published 04/16/22
Hey, Mambo vipi, Leo tutazungumza kuhusu kugoogle au kutafuta majibu ya changamoto unapokuwa kwenye ujenzi wa mfumo. Je, unajisikia vibaya unapogoogle mambo kwenye mtandao kama programmer unanielewa nikisema Stack Overflow. Lakini je, kugoogle kunakufanya wewe kuwa programmer mbaya? Nitakueleza kwa uzoefu wangu pamoja na programmers mashuhuri kabisa ninaowafahamu ambao pia wameshare uzoefu wao katika hili. Nitakueleza pia kuna time unagoogle na hutapata kitu lakini kuna mtu unamjua ana...
Published 03/26/22
Leo tutazungumza kuhusu usalama wa taarifa za kibenki katika kufanya manunuzi online. Technolojia inabadilika kila leo, vilevile maarifa ya kulaghai watumia wa mitandao yazidi kuto tabirika. Mbinu mpya za udukuzi zinaibuka hivyo ni muhimu kutunza vizuri taarifa zako na kuwa makini na watu unaofanya nao biashara kwenye mtandao.
Published 11/09/21
Leo tutazungumza uzoefu wangu katika kufanya manunuzi online sehemu ya pili. Kwenye toleo lilipita nilikueleza maandalizi niliyofanya kabla sijaagizo mzigo. Nilikueleza niliapanga kuagiza mzigo kupitia Amazon na eBay kutokana na maoni mbalimbali niliyopata. Pia njia ya kusafirisha mzigo kupitia MyUs.com na namna nilivyofunga sanduku la posta kiganjani kupitia SmartPosta.
Published 11/01/21
Leo tutazungumza uzoefu wangu katika kufanya manunuzi online. Mid this year niliamua kufanya refresh ya tools ninatumia hapa Yesaya Software (camera, light and mixer) na nilitamani kufanya manunuzi online based on specific models ambazo nilipata recommendations kwa watu wengi online.
Published 10/18/21
Leo nitakushikisha mambo ninayofanya nikiwa sina access ya Internet - yaani bundle limekata. Kwa kawaida nikiwa na internet na niko nyumbani kama siko na watoto basi muda mingi niko kwenye computer. Sometimes sina mood ya kazi basi hapo ndio ninapoteza muda kwenye magroup na Twitter huko. Ila bundle limekata, ninafanya nini? Nitafurahi kusikia pia kutoka kwako, kuna rafiki yangu mmoja amenijubu, baada ya kummuliza anafanya nini bundle likikata, ameniambia ananunua bundle.
Published 10/10/21
Hey, Mambo vipi, Leo nitakupatia update ya kazi niliyofanya this weekend. Nimekamilisha kurekodi na kupublish video 8 kuhusu Laravel Community Website. Na kubwa tunatengeza website hii pamoja, hakikisha unachek kule GitHub kuweza kushiriki ujenzi na pia kule YouTube kwa video tutorials kuhusu development ya hii website. Lakini kabla hatujasonga mbele ninapenda kuchukua fursa hii kukushukuru sana kwa kuweza nifanikisha kufikia download elfu 5 kwenye Yesaya Software Podcast. It means a lot...
Published 09/19/21
Leo tunakwenda kujadili kidogo kuhusu path niliyochukua kutengeneza cross platform apps, hapa ninamaanisha Android and iOS App. Kutokea awali nimekuwa mzito sana kudevelop apps ambazo sio native yaani sio specific kwa Android na iOS. Nina imani toleo hili litakuwa msaada pia kwa wadau mbalimbali wa TEHAMA kujua technolojia zinazohusika kutengeneza Mobile Apps.
Published 09/16/21
Ukweli na Elimu kuhusu YouTube Monetisation
Published 08/14/21
Leo kwenye Twitter Spaces na Yesaya Software tumejadili kuhusu uhusiano wa Mentor na Mentee. Tulijadili mambo mengi ikiwa na kuangalia sababu za kwa nini utahiji mentor.
Published 08/13/21
Kuwa mwangalifu na matumizi ya pesa kwenye mtandao. Kwa maisha ya sasa kwenye mtandao kuna kila kitu tunachohitaji tamaa au uvivu unaweza kukupelekea kutaka kulipia kila kitu kwenye mtandao.
Published 08/12/21
Freelancer kwa miaka mitano nitakusimulia changamoto na fursa. Hii ilikuwa sehemu ya mazungumzo yangu na wadau mbalimbali kwenye Twitter Spaces. Nilipata fursa kusikia uzoefu kutoka kwa Baraka, Justin, Kalebu na Alpha. Unaweza kusikiliza sasa na nina imani kuna jambo utajifunza.
Published 08/11/21
Kwenye toleo hili ni sehemu ya majadiliano kwenye Twitter Spaces na nilijadili na wadau niweke content ya aina gani kwenye mtandao ili niweze kupata traffic. Pia tulizungumza mambo ya kuzingatia kwenye kufanya option ya Voice chat (Twitter Spaces na Clubhouse), Livestream na Podcast. Ungana nasi sasa kusikiliza toleo hili na usiache kuingia pale Twtter @yesayasoftware
Published 08/10/21
Hey Mambo vipi, jina langu ni Yesaya na hii ni Yesaya Software Podcast. Leo ninazungumza na Ally Ndimbo mtalaam wa usalama kwenye mtandao, tumezungumza mengi ikiwa ni pamoja na historia ya usalama kwenye mtandao na sheria zinazotulinda hapa nyumbani Tanzania.
Published 06/27/21
Asante sana kusikiliza Yesaya Software Podcast na Leo ninazungumza na Kaleb Gwalugano. Kaleb ni Software Developer na nilifanya mazungumzo nae kuhusu mchango wake kwenye Open Source community.
Published 06/06/21
Asante sana kusikiliza Yesaya Software Podcast na leo ninazungumza na Marvin Collins kutoka nchini Kenya. Marvin ni Software Developer, sasa kuna mambo machache nilipenda kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu Developers' Community nchini Kenya.
Published 05/29/21
Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Stephen Chacha, Stephen ni Android na Machine Learning Developer kutoka nchini Kenya. Nilifanya majadiliano nae kuhusu Jetpack Compose kama UI toolkit kwenye Android.
Published 05/22/21