UN: Baada ya janga la njaa, sasa kipindupindu na homa ya kidingapopo yaikumba Sudan
Listen now
Description
Nchini Sudan ambako vita na njanga la njaa vinaendelea kuwa mwiba kwa raia  sasa wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanaonya juu ya tishio lingine kubwa  la milipuko ya magonja ya kipindupindu na homa ya kidingapopo huku mfumo mzima wa afya ukiwa taabani.  Asante Assumpta kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA na lile la afya duniani WHO, hali inazidi kuwa mbaya Sudan ambako katikati ya vita majanga mingine ya kiafya yanazuka. OCHA imeripoti zaidi ya wagonjwa 28,000 wa kipindupindu na vifo vimefikia 836 katika majimbo 11 kati ya 22 Julai na 28 Oktoba mwaka huu huku likihofia kwamba idadi kamili ya wagonjwa huenda ni kubwa zaidi. Pia shirika hilo limeonya juu ya kuendelea kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa homa ya kidingapopo na mvua zinazonyesha na kusababisha mafuriko makubwa zimeongeza hatari ya kusambaa kwa magonjwa hayo. Nalo shirika la WHO linasema milipuko hii imezuka wakati mfumo wa huduma ya afya nchini Sudan umzidiwa uwezo, huku hospitali nyingi hazifanyi kazi au zimefungwa kabisa kutokana na usambazaji mdogo wa vifaa na uhaba wa mafuta. Shirika hilo linasema hadi asilimia 80 ya vituo vya afya katika maeneo yenye migogoro ikiwa ni pamoja na Al Jazirah, Kordofan, Darfur na Khartoum  aidha havifanyi kazi au vimefungwa. Na linaonya kwamba "Kuporomoka huku kwa mfumo  wa afya  kunazuia mipango ya chanjo ya watoto,  kuongeza kasi ya kuenea kwa magonjwa yanayozuilika, na kuzua wasiwasi kuhusu uwezekano wa milipuko mikubwa zaidi ya magonjwa." Kwa sasa mashirika hayo yamesema majimbo yaliyoathirika zaidi na kipindupindu ni Kassala Gedaref, Al Jazirah, na Northern wakati homa ya kidingapopo imeghubika zaidi majimbo ya Kassala na Khartoum. Pia changamoto nyingine kubwa ya kutoa huduma za afya katikati ya milipuko hii mashirika hayo yanasema ni mashambulizi dhidi ya vituo vya afya ambayo tangu kuanza kwa vita 15 Aprili mwaka jana  yamefikia 116 na kusababisha vifo 188 na majeruhi 140.
More Episodes
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na...
Published 11/26/24
Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia...
Published 11/26/24