04 NOVEMBA 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Sudan unaosababisha janga la njaa, na mradi wa maji Galmudug Somalia kwa ajili ya maji safi na salama pamoja na mifugo. Makala tunakupeleka nchini DR Congo na mashinani nchini Kenya, kulikoni? Nchini Sudan ambako vita na janga la njaa vinaendelea kuwa mwiba kwa raia      sasa wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanaonya juu ya tishio lingine kubwa  la milipuko ya magonja ya kipindupindu na homa ya kidingapopo huku mfumo mzima wa afya ukiwa taabani.Nchini Somalia, ni asilimia 52 tu wananchi ndio wanapata huduma ya maji safi na salama. Wengine hulazimika kutembea umbali mrefu kuteka maji ambayo si ya uhakika. Hata hivyo kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo pamoja na wadau, hali sasa inaanza kuimarika.Makala inakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako Kapteni Fadhillah Nayopa, Afisa habari wa kikosi cha 11 cha walinda amani wa Tanzania, TANZBATT-11 katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO anazungumzia usaidizi waliopatia watoto yatima.Mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula, tunakutana na Geoffrey Nawet, Mwanafunzi katika shule ya Kakuma nchini Kenya akitueleza jinsi ambavyo programu ya Mlo shuleni ya lishe bora umewawezesha wanafunzi kumakinika shuleni na kupata motisha ya kuendelea na masomo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
More Episodes
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na...
Published 11/26/24
Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia...
Published 11/26/24