Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia uvuvi katika mji wa Kalokol karibu na fuo za Ziwa Turkana Kaskazini mwa Kenya. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za mkutano wa WUF12 Cairo Misri, chanjo ya malaria Sudan, siku ya Tsunami, na mashinani.
Mkutano wa 12 wa Jukwaa la Miji Duniani, WUF12 umeingia siku ya pili hii leo huko Cairo, Misri, ambako Ming Zing ambaye ni Mkurugenzi wa Miji, Mnepo na Ardhi kutoka Benki ya Dunia amezungumzia umuhimu wa kujumuisha wanawake na vijana katika mipango miji.Sudan imekuwa nchi ya 16 barani Afrika na ya kwanza katika Ukanda wa WHO wa Mashariki na Mediterania kuanzisha chanjo dhidi ya Malaria kwa watoto wasiozidi umri wa miezi 12. Chanjo imeanza kutolewa jana katika majimbo ya Gedaref na Blue Nile ambapo WHO na wadau wamesema mwaka 2025 na 2026 chanjo itapelekwa katika maeneo 129 nchini kote Sudan.Na leo ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha umma kuhusu tsunami, ambayo ni mawimbi makubwa ya maji yatokanayo na tetemeko chini ya bahari. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake anasema pamoja na kukumbuka waliopoteza maisha kwa tsunami miaka 20 iliyopita, tunaahidi tena kulinda zaidi ya watu milioni 700 duniani kote walio hatarini kukumbwa na Tsunami.Mashinani tutaelekea Sudan kusini kuangazia harakati za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo, UNMISS za kuimarisha ulinzi wa wanawake katika migogoro na majanga.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na...
Published 11/26/24
Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia...
Published 11/26/24