07 NOVEMBA 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka huko Havana Cuba kwenye Kongamano la kimataifa la Kiswahili kusikia kutoka kwa waziziri Zanzibar kuhusu faida za kiplomasia na kiuchumi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ujumbe kuhusu Kiswahili. Fedha kwa ajili ya mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ni jambo lililopatiwa kipaumbele katika ripoti mpya ya leo ya shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP wakati huu ambapo kiwango cha joto kinazidi kuongezeka kila uchao na kuleta zahma duniani kote.Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO linasema hii leo watoto 6 wa kipalestina, wamesafirishwa kutoka Gaza kwenye Romania kwa matibabu mahsusi ; watatu wakiwa wanaugua saratani, wawili magonjwa ya  damu na mmoja majeraha. Wameambatana na jumla ya waangalizi 15.Na huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO umezindua mfumo wa uthibitishaji, kama sehemu ya mchakato wa Luanda wenye lengo la kufuatilia makubaliano ya sitisho la mapigano kati ya Rwanda na DRC yaliyoanza kutekelezwa tarehe 4 mwezi Agosti mwaka huu mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunasalia huko huko Havana Cuba, kwenye kongamano la Kiswahili la Kimataifa ambako Dkt. Kisembo Ronex Tendo mshiriki kutoka taasisi ya vijana ya Afrika Mashriki Fest Uganda anaeleza cha kufanya kusongesha Kiswahili nchini Uganda.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
More Episodes
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na...
Published 11/26/24
Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia...
Published 11/26/24