08 NOVEMBA 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunakuletea kipindi maalum kinachotupeleka jijini Havana Cubaambapo kongamano la kimataifa la Kiswahili limeng’oa nanga likiwaleta pamoja takribani washiriki 400 kutoka Afrika, Asia, Amerika na Ulaya ili kujadili ajenda mbalimbali za kupanua wigo wa luugha hiyo na kuitumia kuleta tija ikiwemo kusongesha malengo ya Umoja wa Mataifa kama amani na maendeleo endelevu. Miongoni mwa habari kubwa Umoja wa Mataifa hii leo ni uwajibikaji unasakwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya  wapalestina na waisraeli, na pia shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limeweka bayana gharama za kiuchumi na hata kiafya zilizofichika zitokanazo na mifumo ya uzalishaji, usafirishaji na ulaji wa chakula. Lakini kubwa zaidi nakupeleka Havana, Cuba kupata kwa mahtasari mazungumzo ya Flora Nducha na mmoja wa washiriki. Mashinani tunasalia huko huko Havana Cuba na fursa ni yake Profesa Juan (Huani) Jacomino (Hakumino) raia wa Cuba ambaye ni Mwalimu wa Kiswahii katia  chuo kikuu cha Havana Cuba anayeshiriki Kongamano la Kiswahili lililofunguliwa leo akitoa wito kwa raia wa Cuba na wa nchi zingine kuhusu umuhimu wa kukumbatia  Kiswahili.  Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu! 
More Episodes
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na...
Published 11/26/24
Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia...
Published 11/26/24