Stiell: Lazima tuweke malengo ya juu ya ufadhili ili kukabili mabadiliko ya tabianchi
Listen now
Description
Kufuatia mwaka mwingine wa viwango vya juu vya joto kali na matukio ya kupitiliza ya hali ya hewa, Mkuu wa Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Tabianchi Simon Stiell amewaeleza washiriki wa mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 , kwamba malengo mapya ya ufadhili kwa tabianchi ni muhimu kwa ajili ya ustawi wa mataifa, yakiwemo yale tajiri na yenye uthabiti.  Katika hotuba yake mbele ya washiriki wa mkutano huo ulioanza leo huko Baku, mji mkuu wa Azerbaijan hadi tarehe 22 mwezi huu wa Novemba, Bwana Stiell amesema kwa kadri madhara ya mabadiliko ya tabianchi yalivyo dhahiri ni lazima kukubaliana mwelekeo mpya wa ufadhili kwa miradi ya kukabili na kuhimili. Amehoji, mnataka bei za vyakula na nishati iongezeke zaidi? Je mnataka nchi zenu ziendele kushindwa kushindana kiuchumi? Je mnataka dunia yetu iendelee kukosa utulivu na kugharimu maisha adhimu? Amekumbusha kuwa janga la tabianchi linaathiri kila mkazi wa dunia kwa njia moja au nyingine. Bwana Stiell amesema nimekanganyikiwa kama mtu mwigine yeyote kwamba mkutano mmoja wa COP hauwezi kuleta marekebisho abayo kila taifa linahitaki. Lakini iwapo majibu yenu kwenye maswali hayo ni HAPANA, basi ni hapa pande zote zinahitaji kukubaliana jinsi ya kuondokana na zahma hii. Hivyo amesema, “katika nyakati ngumu, kukiwa na majukumu mazito, sitegemei matumaini na ndoto. Kinachonihamasisha ni stadi na azma ya binadamu. Uwezo wetu wa kuanguka na kuinuka tena na tena, hadi tunapotimiza malengo yetu.” Amekumbusha kuwa mkataba wa tabianchi ndio mchakato pekee ambapo wanaweza kupatia majawabu janga la tabianchi na kuwajibishana kwa wale wanaokwenda kinyume. Ametaka washirika kuonesha stadi zao kwenye COP29 na pande zote zishinikize makubaliano ya ufadhili kwa tabianchi la sivyo kila nchi itagharimika.
More Episodes
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na...
Published 11/26/24
Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia...
Published 11/26/24