11 NOVEMBA 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunaangaziamkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29, na mradi wa lishe bora kwa watotot Afar nchini Ethiopia. Makala inatupeleka Havana Cuba na mashinani tunasalia huko huko Havana Cuba, kulikoni? Kufuatia mwaka mwingine wa viwango vya juu vya joto kali na matukio ya kupitiliza ya hali ya hewa, Mkuu wa Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Tabianchi Simon Stiell amewaeleza washiriki wa mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29, kwamba malengo mapya ya ufadhili kwa tabianchi ni muhimu kwa ajili ya ustawi wa mataifa, yakiwemo yale tajiri na yenye uthabiti.Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kuchagiza kaya kulima bustani za mboga za majani pamoja na ufugaji wa kuku huko jimbo la Afar, kaskazini mashariki mwa Ethiopia umesaidia familia za vijijini kukabiliana na utapiamlo miongoni mwa watoto.Makala inatupeleka Havana Cuba ambako kongamano la kimataifa ka Kiswahilii limekunja jamvi mwishoni mwa wiki na shuhuda wetu huo Flora Nducha amezungumza na watu mbalimbali akiwemo mchechemuzi wa Kiswahili hususan kwenye mitandaao ya kijamii Nick Reynold ali maarufu Bongo Zozo, ambaye ni raia wa Uingereza.Na mashinani fursa ni yake Profesa msaidizi Xiaoxi Zhang raia wa China ambaye ni mshirika wa kimataifa au (Global Fellow) na mhadhiri wa masuala ya fasihi linganishi katika chuo kikuu cha Habib kilichopo Sindhi Karachi nchini Pakistan mmoja wa waliohudhuria kongamano la Kiswahili lililomalizika mwishoni mwa wiki akitoa ujumbe kuhusu changamoto ya kujifunza  Kiswhili.Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu! 
More Episodes
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na...
Published 11/26/24
Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia...
Published 11/26/24