Mradi wa UNICEF wa kuboresha lishe waleta tabasamu kwa wazazi na watoto Afar Ethiopia
Listen now
Description
Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kuchagiza kaya kulima bustani za mboga za majani pamoja na ufugaji wa kuku huko jimbo la Afar, kaskazini mashariki mwa Ethiopia umesaidia familia za vijijini kukabiliana na utapiamlo miongoni mwa watoto.  Video ya UNICEF Ethiopia inaanza ikimuonesha mtoto akitabasamu, na kisha akiwa na mama yake wakielekea kwenye kituo cha afya. Mama huyu anaitwa Fatuma Kebir na mwanae huyu aliyembeba anaitwa Abdu. Fatuma anasema.. “Nilihofia kuwa angeendelea kuwa na utapiamlo. Kwa hiyo nilimpeleka kituo cha afya na mhudumu wa afya akanieleza kuwa mwanangu amepoteza uzito, kama ambavyo nilihisi. Akaniambia nimlishe zaidi, hasa uji uliochanganywa na mayai, maziwa, na mboga.” Video ikimuonesha Fatuma akiandaa uji akichanganya na mayai, mtaalam wa lishe wa UNICEF, Yetayesh Maru, anasema, “Kama sehemu ya mtambuka wa hatua na uratibu dhidi ya utapiamlo kwenye jamii, Fatuma ametambuliwa kuwa ni kaya iliyo hatarini, hivyo amenufaika na mradi wa kisekta wa kuboresha lishe kwa watoto.” Sasa Fatuma na mtoto wake Abdu wanapata tabasamu upya. “Nilimlisha kwa mwezi mmoja kama walivyoshauri na kisha nikarudi kituo cha afya. Mtoa huduma alisema kwamba sasa ana afya na amerudia uzito wake. Nilifurahi sana alipoanza kuongezeka uzito.” Tabasamu lao ni dhahiri hata kwa mtoa huduma Yetayesh, akisema “Sasa Abdul anakua vizuri, na nguvu kamilifu, huku akicheka na mama yake.”
More Episodes
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na...
Published 11/26/24
Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia...
Published 11/26/24