14 NOVEMBA 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Baku kwa mkutan wa COP29, amabyo washiriki wanasaka mbinu za kujumuisha makundi yote katika harakati za kukabili na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayochochewa na ongezeko la hewa chafuzi. Idhaa ya Kiswahili imezungumza na Naomi mmjoja wao kutoka Tanzania. Pata pia muhtasari wa habari na ujifunze Kiswahili. Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa kisukari, shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO leo limesema idadi ya watu wazima wanaoishi na Kkisukari duniani ni zaidi ya milioni 8000 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara 4 tangu mwaka 1990.Baku Azerbaijan ambako mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 leo umejikita na na lengo la kutozalisha kabisa hewa ya ukaa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antinio Guterres ameainisha jukumu muhimu ambalo miji, mikoa, biashara na taasisi za kifedha lazima zitekeleze katika kuendesha juhudi za dunia nzima kufikia lengo la kutozalisha kabisa hewa ya ukaa katikati ya karne hii.Nchini Sudan shirika la Umojja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharida OCHA limesema ghasia za kutumia silaha na mashambulizi katika Jimbo la Aj Jazirah zinadhihirisha ukatili wa karibu miezi 19 ya vita nchini Sudan,huku kukiwa na ripoti za ubakaji, mauaji ya halaiki na uporaji mkubwa. Katika chini ya wiki mbili, OCHA inasema uhasama huko Aj Jazirah umefurusha zaidi ya watu 135,000 kutoka makwao, wengi wao walikimbilia majimbo jirani ya Gedaref na Kassala.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “MADHALI, WAMA, FALAU NA HOBE”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
More Episodes
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na...
Published 11/26/24
Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia...
Published 11/26/24