Description
Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa ndani nchini Haiti, na mafunzo ya stadi za kujikimu kimaishwa kwa vijana Tambura Sudan Kusini. Makala inatupeleka nchini Uganda na mashinani nchini Kenya, kulikoni?
Zaidi ya watu 20,000 wamekimbia makazi yao katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince katika muda wa siku nne tu, ikiwa ni pamoja na watu wengine zaidi ya 17,000 wanaohifadhiwa katika makazi 15 ya wakimbizi wa ndani, kutokana na kuongezeka kwa ghasia za magenge ya uhalifu ambazo ziumevuruga kabisa minyororo muhimu ya usambazaji wa misaada na kulitenga jiji la Port-au-Prince limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.Vijana katika mji wa Tambura ulioko jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wanageuza mafunzo ya ufundi stadi kuwa nguvu ya amani na ustawi, mafunzo ambayo yalifanikishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS.Katika makala Selina Jerobon kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi anakupeleka Uganda kuona harakati za wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kujikwamua kiuchumi baada ya machungu waliyopitia nyumbani kwao.Mashinani tutaelekea nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani jamii katika maeneo kame wanakabiliana na mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Bosco Cosma, karibu!
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na...
Published 11/26/24
Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia...
Published 11/26/24