Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Baku nchini Azerbaijan kwenye mkutano wa COP29. Miongoni mwa mambo yanayopigiwa chepuo ni madini ya kimkakati yanayoelezwa kuwa ni jawabu la nishati chafuzi kwa mazingira na tunapata ufafanuzi kutoka kwa Adam Anthony, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali nchini Tanzania.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewasihi viongozi wa kundi la nchi 20 zenye uchumi mkubwa zaidi duniani, G20 wanaokutana huko Rio De Janeiro, Brazil kuwaagiza mawaziri na washawishi wao huko COP29 wahakikishe wanakubaliana juu ya lengo jipya na kubwa la mwaka huu la ufadhili kwa tabianchi nchi. Guterres amesema sambamba na hilo ni vema kukabiliana na taarifa potofu kuhusu tabianchi.Huko Kusini mwa Lebanon, walinda amani wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha Mpito nchini humo, UNIFIL, wameshuhudia uharibifu mkubwa wa kutisha kwenye vijiji vilivyoko sambamba na eneo la kati ya Israeli na Lebanon lisilopaswa kuwa na mapigano, huku hali ya watoto nchini humo ikizidi kuwa mbaya.Hii leo ni siku ya choo duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema licha ya choo kuwa ni msingi wa kusongesha afya ya binadamu na kusaidia watoto wa kike na wanawake kuishi maisha ya utu, bado wakazi wengi wa dunia hususan kwenye mizozo na majanga wanaishi bila huduma hiyo ya msingi.Mashinani tunasalia huko huko Baku, kwenye COP29 ambapo nampisha msichana mwanaharakati wa mazingira kutoka Tanzania, akieleza ni nini anafanya na nini atakachoondoka nacho kwenye mkutano huo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na...
Published 11/26/24
Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia...
Published 11/26/24