22 NOVEMBA 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunaangazia majadiliano huko Baku Azerbaijan kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi, na kazi za walinda amani kutoka Tanzania TANZBATT-11 huko DRC. Makala inaturejesha kataika mkutano wa COP29 na mashinani inatupeleka Namibia, kulikoni? Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea.Umoja wa Mataifa unasema kwamba vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imefanya taifa hilo kuwa pahala hatari zaidi duniani kwa watoto kuishi, kutokana na mateso ya kimwili na kisaikolojia wanayoyapitia. Kwa kutambua hilo walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa UN nchini humo, MONUSCO wamechukua hatua kuona watoto wanaishi kama watoto.Makala inakupeleka Baku nchini Azerbaijan kunakotamatika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 kumsikia kijana kutoka Tanzania akizungumzia kilichompeleka, anachoondoka nacho na ujumbe wake kwa  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.Na katika mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, tunasikia kauli ya Willem Westhuizen, mkulima kutoka Namibia, akielezea changamoto zinazotokana na ukame unaoathiri maisha yao kila siku”.  Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu! 
More Episodes
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na...
Published 11/26/24
Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia...
Published 11/26/24