Gumzo la Wiki Podcast: Waiguru ahamia UDA; OKA yapinga kugawika
Listen now
Description
Gavana wa Kirinyaga, Ann Waiguru aigura Jubilee na kujiunga na UDA. Je, Ruto atamchagua kuwa mgombea mwenza? Je, ataweza kumenyana na Purity Ngurici na Martha Karua? Vilevile, Wakenya wamkumbusha Kenyatta ahadi ya kutoa mwanga zaidi kuhusu ufichuzi wa Pandora Papers. Aidha, Mudavadi na Kalonzo watakiwa kuweka wazi misimamo yao kuhusu kinyang'anyiro cha urais mwaka ujao. Watakwenda hadi debeni au la? Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraise wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshirika gumzo na Wakenya kuhusu masuala haya.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu...
Published 11/05/22