Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha kutoka Marekani kupiga jeki Hazina ya Hustler Fund. Umesaidika na fedha hizo? Kiwango ulichoomba kimeongezeka? Pia kuna masaibu ya Cherera4. Unasemaje kuwahusu? Tribunal iendelee kuwachunguza au unasema...
Published 12/17/22
Published 12/17/22
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu ya Tinga Kenya Kwanza, Tinga naye anasema wewe kijana wacha kuniota kila saa mimi si rika lako. Unamshauri vipi Riggy G? Vilevile Baba anataka Waluke kuachiliwa huru. Eti kesi dhidi yake itupiliwe...
Published 11/05/22
GMO imezua gumzo, Azimio wakipinga. Kalonzo naye anasema Rais Ruto analenga kuangamiza kilimo cha mimea ya kiasili. Mbali na hayo, unadhani kwamba Kalonzo anatoshea viatu vya Odinga katika upinzani? Baba naye angali anamlaumu Chebukati na mataifa ya kigeni, kwamba yaliingilia uchaguzi wa Kenya! Unasemaje? Si hayo tu, Azimio inasema Ruto amekuwa kiguu na njia, bila kwanza kutimiza ahadi kwa Wakenya. Nawe unatathmini vipi utendakazi wa Ruto ndani ya siku 30 tangu kuapishwa? Wanahabari wetu...
Published 10/14/22
Mgombea urais wa UDA, William Ruto amezindua manifesto yake akiangazia nguzo sita; kupunguza gharama ya maisha, kumaliza uhaba wa walimu, matibabu bila malipo, kujenga nyumba elfu 250 kila mwaka, kukuza biashara na kuimarisha kilimo. Ahadi hizi zinatekeleka? Upande mwingine Wajackoyah ameweka wazi manifesto yake akijumuisha mambo ya kiajabu. Mara atahamisha jiji la Nairobi hadi Isiolo, sijui kufuga nyoka, kuvunja sekta ya bodaboda na kuwaajiri wahudumu hao katika mashamba ya bangi na mengine...
Published 07/02/22
Nyumba ya Kenya Kwanza imeanza kuwaka moto. Kuria na Kabogo wataka mkutano wa dharura wakimshtumu Gachagua kufuatia madai ya udikteta. Aidha, wanadai wana-UDA wanapendelewa katika kampeni za Kenya Kwanza. Kunani? Gachagua amekuwa mzigo Kenya Kwanza? Anavutia kura au anafukuza? Sakata ya Sakaja kuhusu digrii nayo yamfikia Tinga na Hustler. Kelele zimechacha kuhusu kisomo cha Tinga na PHD ya Hustler. Baba awataje classmates wake. Bei za mafuta zimeendelea kupanda. Tuwalaumu nani? Wanahabari...
Published 06/18/22
Bunge la 12 limevunjwa rasmi baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitano. Je, limetimiza matarajio ya Wakenya ama limekuwa bunge la demokrasia ama utumbokrasia kwa kujali tu donge nono kupitia marupurupu? Kura za maoni nazo zinaendelea kutolewa kuelekea uchaguzi mkuu. Je, ni za kuaminika ama zinatoa taswira ya kila mwamba ngoma kuvutia kwake? Raila Odinga naye ametangaza manifesto ambayo imeibua gumzo kuu hasa kwa kuzitaja nguo za mitumba kuwa za wafu yaani marehemu. Je, alieleweka...
Published 06/10/22
Wasifu wa Hayati Stanly Emilio Mwai Kibaki aliyeongoza Kenya kati ya 2002 - 2012 na kuaga dunia tarehe 22/04/ 2022. Wasifu huu umeandaliwa na kusimuliwa na Victor Mulama.
Published 04/23/22
Mchujo wa vyama vya kisiasa unapoendelea, lipo jambo moja bainifu kuhusu matokeo kuhusu ngome za Naibu wa Rais William Ruto kulinganishwa na ngome ya Raila Odinga. Kwenye eneo la Bonde la Ufa ambako Ruto ana ufuasi mkubwa, baadhi ya wanasiasa wenye tajriba wamelambishwa sakafu huku vijana wengi wakiingia ulingoni. Na huko Nyanza, wanasiasa wengi waliokuwapo uongozini wamedumishwa hasa katika nyadhifa za ubunge, useneta na ugavana. Aidha, katika ngome zote mbili, idadi kubwa ya wawakilishi...
Published 04/20/22
Uchaguzi mkuu unapokaribia kila chama cha kisiasa kinaweka mikakati ya kuhakikisha mchujo utaofanyika katika chama unakuwa huru na wa haki. Mkurugenzi Mkuu katika Chama cha UDA, Odanga Pesa vilevile Cathrene Muma ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uchaguzi ya ODM wanazungumzia mikakati mbalimbali inayofanywa na vyama vyao kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Published 02/19/22
Baada ya kimya kingi na fukuzafukuza chamani, hatimaye Rais Uhuru Kenyatta amefanya mkutano na viongozi wa Jubilee katika Ikulu. Ikumbukwe chama hicho kimepanga Mkutano wa Kitaifa wa Wajumbe, NDC tarehe 25 Februari, 2022 katika Ukumbi wa KICC, mjadala ukiwa kuwafurusha rasmi Ruto na wandani wake kutoka chama hicho, mpango wa kushirikiana na miungano mingine na kumfanyia kampeni Raila Odinga. Vilevile mjadala mkali umechacha kuhusu mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi. Wana-OKA nao baada ya pigo...
Published 02/05/22
Katika Ukweli wa Mambo leo, tunaangazia hotuba ya Musalia Mudavadi wakati Kongamano la Kitaifa la ANC, Januari 23 mwaka wa 2022. Je, aliyoyasema yana ukweli ama la na kwa kiwango gani? Huu hapa ukweli wa mambo baada ya utafiti wa kina baina ya Shirika la Habari la Standard kwa ushirikiano na kampuni ya Africa Check. Katika hotuba yake ya kipekee ya kukubali uteuzi wa kupeperusha bendera ya urais kupitia chama chake, Musalia aliahidi kufufua uchumi jinsi alivyofanya alipokuwa Waziri wa Fedha...
Published 01/31/22
Mjadala mkali umetawala vinywa vya wengi wiki hii, kufuatia hatua ya Mudavadi na Wetangula kujiondoa katika OKA na kuungana na Ruto. Hatua hiyo imechochea gumzo huku wengi wakijiuliza je, Ruto atavuna kura nyingi za Magharibi dhidi ya Raila? Hatima ya Kalonzo katika OKA ni gani hasa? Atawania urais, ama ataungana na Raila katika Azimio la Umoja? Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wanaangazia makala hapa.
Published 01/29/22
Earthquake aliyoahidi Musalia Mudavadi inasubiriwa kwa hamu kuu Jumapili. Amewaalika wana'OKA na kuwafungia nje Ruto na Raila. Wakenya wana maoni gani? Aidha, cheche baina ya Raila na Ruto zimezidi, kuhusu urushaji mawe na kuitana majina. Haya yanahatarisha utangamano nchini? UDA tayari imeandikia ICC ikidai serikali inafadhili vurugu kwa manufaa ya Raila. Vilevile tunaangazia kesi ya BBI katika Mahakama ya Juu. Je, reggae itarejea? Kadhalika tunazamia suala la mili katika Mto...
Published 01/22/22
Benson Cheserek ni miongoni mwa Wakenya ambao wanaishi ughaibuni (Kenyans in diaspora) na sasa analenga kuwania kiti cha ubunge kwenye eneo la Marakwet Magharibi katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet. Cheserek amekuwa akiishi Marekani kwa miaka 17 ambapo amefanya kazi katika jeshi la Marekani kwa miaka 8 kabla ya kuanza biashara yake binafsi. Kwenye mahojiano na mwanahabari Faith Kutere, Cheserek anasema analenga kutumia ujuzi wake katika idara ya usalama kusaidia kukabili ukosefu wa usalama...
Published 01/18/22
Wanasiasa kadhaa wamekamatwa kwa kuhusishwa na matamshi ya uchochezi. Swali ni je, kuna mapendeleo jinsi UDA inavyodai? Je, ni kamatakamata kwa kigezo cha mirengo ili kuleta usawa wa kisiasa? Aidha, Rais Kenyatta alifanya mkutano katika Ikulu na viongozi wanaounga mkono Azimio la Umoja akiwamo Raila ambapo wote walipigia debe Mswada wa Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Kisiasa. Vigogo wa OKA walisusia mkutano huo wa Ikulu, licha ya kualikwa. Je, hatua yao inatoa picha gani?Vilevile,...
Published 01/15/22
Mswada wa Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Kisiasa umekuwa kichocheo cha mjadala wiki hii, ambapo wengi wanajiuliza iwapo kufaulu kwake kutakuwa mwanzo wa wanasiasa kuaminiana. Je, iwapo mswada huo utafanywa sheria, tutarajie miungano gani, hasa kati ya nani na nani? Na je, mswada huu umeashiria upande gani kuwa na ubabe bungeni? Aidha, tunaangazia mwaliko wa Ruto kwa kina Mudavadi na Wetangula licha ya kusema hawajaalikwa wala kukutana na yeyote kujadili miungano. Je, kuna karata...
Published 01/09/22
Mjadala mkali unaendelea kufuatia hatua ya Raila Odinga kuwatafuta marafiki wapya wa kisiasa, hasa kwenye eneo la Magharibi baada ya Mudavadi kusisitiza kwamba hatamuunga mkono tena. Aidha, Ruto anawataka Mudavadi na Wetangula wajiunge naye katika UDA. Si hayo tu, ipo hofu kutokana na kupanda kwa maambukizi ya korona hasa baada ya kugunduliwa kwa Omicron hapa Kenya. Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraise wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na...
Published 12/20/21
Kauli ya Rais Kenyatta kuwa Kenya ni namba sita barani Afrika kwa utajiri imewaghadhabisha Wakenya wanaosema umaskini umekithiri nchini. Kuhusu siasa, Rais Kenyatta anasema wanasiasa viana watashindwa na wazee licha ya mbio zao za kisiasa. Je, sasa ni wazi kuwa Uhur anamuunga mkono Odinga kuwania urais? Je, hatima ya OKA ni gani? Aidha, IEBC imejiondoa katika kamati ya pamoja ya maandalizi ya uchaguzi. Maoni yako ni gani? Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri na Moses Kiraise wa Pokot...
Published 12/05/21
Naibu wa Rais William Ruto abebeshwa lawama kuhusu vuruga za Kondele. Je, vuruguzu hizo zilichochewa kisiasa anavyodai? Na je, Ruto alifanya makosa kumshtumu Odinga katika ngome yake? Adha, Wakenya wanahisi kwamba Kalonzo Musyoka amekosa mwelekeo na wakati umefika kwake kutangaza wazi msimamo wake wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Vilevile, Nick Mwendwa atakiwa kueleza jinsi amekuwa akiendesha shughuli za FKF. Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Washington Onyango wa Kisumu na Moses...
Published 11/14/21
Imekuwa wiki yenye matukio kadhaa ya kisiasa huku muungano wa OKA ulioonekana kufifia ukifufuka kwa mikutano ya kuwatia wasiwasi wapinzani japo swali ni lile lile la ni nani atakayepata tikiti? Kule Jubilee, mikakati ya kumtema Ruto rasmi inaendelea huku naye akiendeleza cheche kali, wakati huu akikosoa mikopo waliyoichukua kwa pamoja na Rais Kenyatta. Wanafunzi nao wamefanikiwa kuishinikiza serikali kuwapa likizo. Ndiyo suluhu ya mioto shuleni? Moses Kiraese wa Pokot Magharibi, William...
Published 11/07/21
Gavana wa Kirinyaga, Ann Waiguru aigura Jubilee na kujiunga na UDA. Je, Ruto atamchagua kuwa mgombea mwenza? Je, ataweza kumenyana na Purity Ngurici na Martha Karua? Vilevile, Wakenya wamkumbusha Kenyatta ahadi ya kutoa mwanga zaidi kuhusu ufichuzi wa Pandora Papers. Aidha, Mudavadi na Kalonzo watakiwa kuweka wazi misimamo yao kuhusu kinyang'anyiro cha urais mwaka ujao. Watakwenda hadi debeni au la? Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraise wa Pokot Magharibi na Martin...
Published 10/31/21
Kuondolewa kwa marufuku ya kuwa nje kwashabikiwa na Wakenya. Aidha, Mt. Kenya yasubiri ahadi ya Uhuru kuhusu kilichomkosanisha yeye na Ruto. Huko Kisii, hulka ya kuwateketeza wazee kwa madai ya kushukiwa kuwa wachawi yazua ghadhabu na kauli kinzani. Wanahabari wetu, John Mbuthia, William Omasire na Martin Ndiema wamewashirikisha wananchi kuhusu haya.
Published 10/24/21
Vikao vya Wafanyabiashara wa Mount Kenya Foundation vimetikisa siasa za Kenya wiki hii, baada ya kusema wataamua kuhusu mgombea wa urais watakayemuunga mkono miongoni mwa vigogo wa OKA na Raila. Je, ajenda ya wafanyabiashara hao ni kumkabili Naibu wa Rais, William Ruto au ni kupigania maslahi ya wakazi wa Mlima Kenya? Aidha, ufichuzi wa Pandora Papers umeibua maswali mengi kuhusu uzalendo wa Kenyatta na uhalali wa mali fiche na akaunti zake za siri nje ya Kenya. Je, ufichuzi huo...
Published 10/10/21
Kuidhinishwa kwa Gideon Moi kupeperushwa bendera ya KANU kumezidisha ushindani wa urais kuelekea 2022. Aidha, Rais Kenyatta anawawinda wana-OKA usiku na mchana ili wote waseme Mzee Tinga tosha. Na je, wabunge wa Kieleweke watafaulu kumfanyia Odinga kampeni Mlima Kenya? Nao wandani wa Ruto wanasema wafanyabiashara wa Mt. Kenya Foundation hawana usemi wa kisiasa. Vilevile tumeangazia Mswada wa NHIF na mpango wa Afya kwa Wote, UHC? Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraese wa Pokot...
Published 10/02/21