Gumzo la Wiki Podcast: Mt. Kenya Foundation ina ushawishi wa kisiasa?
Listen now
Description
Vikao vya Wafanyabiashara wa Mount Kenya Foundation vimetikisa siasa za Kenya wiki hii, baada ya kusema wataamua kuhusu mgombea wa urais watakayemuunga mkono miongoni mwa vigogo wa OKA na Raila. Je, ajenda ya wafanyabiashara hao ni kumkabili Naibu wa Rais, William Ruto au ni kupigania maslahi ya wakazi wa Mlima Kenya? Aidha, ufichuzi wa Pandora Papers umeibua maswali mengi kuhusu uzalendo wa Kenyatta na uhalali wa mali fiche na akaunti zake za siri nje ya Kenya. Je, ufichuzi huo utasaidia kukabili ufisadi nchini? Na je, Wakenya wanahisi vipi kuhusu matokeo duni ya Timu ya Taifa ya Harambee Stars? Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraese wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki Gumzo na wakazi wa maeneo yao kuhusu masuala haya.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22