Episodes
Je, ni kweli kuwa BBI ilichangia kukwama kwa miradi ya maendeleo? Kuna haja ya Rais Kenyatta na Odinga kuwaomba Wakenya msamaha kwa kuhujumu maendeleo kupitia BBI jinsi anavyodai Naibu wa Rais, William Ruto? Na je, ni sawa kwa Kenyatta na Odinga kumlaumu Ruto kwa kuchangia kuanguka kwa BBI au ni visingizio tu? Aidha, siasa za eneo la Kati zinazidi kuwa ngumu, Martha Karua akiteuliwa kuwa Msemaji wa Mt. Kenya Unity Forum. Ataweza? Huko Kirinyaga, Gavana Ann Waiguru aambiwa ahamie UDA ili...
Published 09/26/21
Suala la usalama huko Laikipia linazidi kuwa kero huku wanasiasa wakilaumiwa kuchochea hali hiyo. Je, nani wa kulaumiwa kufuatia kudorora kwa usalama? Ruto naye amemjibu Matiang'i kuwa iwapo anadhani ana ardhi Laikipia, basi awagawie wakazi. Katika ulingo wa siasa, Mlima Kenya imekuwa kama msichana mrembo anayemezewa mate huku kila anayetaka kuwania urais akitafuta mgombea mwenza huko. Nani awe mgombea mwenza wa nani? Aidha, viongozi wameanza ujanja wa kuwa karibu na Mkenya huku Raila...
Published 09/12/21
Suala la usalama wa Naibu wa Rais, William Ruto limezua mjadala mkali wiki hii na hata kugeuka kuwa mazungumzo ya kulinganisha mali anayomiliki Ruto dhidi ya viongozi wengine. Aidha, maswali mengi yameibuliwa kufuatia jinsi Waziri wa Usalama, Dkt. Fred Matiang'i alivyotumia vikao vya bunge kutangaza mali ya Ruto hasa inayolindwa na maafisa wa usalama. Je, unadhani hatua hiyo imemmaliza au ndiyo imemjenga Ruto kisiasa? Vilevile siasa za Mlima Kenya zinazidi kushika kasi huku baadhi ya...
Published 09/08/21
Suala la kuzuiwa kwa Ruto kwenda Uganda linazidi kuzua gumzo, taifa hilo likisema halikufahamu kuhusu ziara hiyo. Karanja Kibicho naye anasema ofisi yake haikuwa na habari. Nani hasa aliyepiga simu Ruto azuiwe? ODM nayo inasema Ruto alilenga kwenda Uganda kujifunza namna ya kutwaa uongozi kwa nguvu ama kukatalia madaraka. Je, bottom up ni ya kuinufaisha Uganda jinsi inavyodai ODM? Naye Murathe amewasisitizia Wakenya kwamba Raila ndiye atakayekuwa Rais 2022. Murathe anajua siri gani ya...
Published 08/08/21
Suala la polisi kupewa ushauri nasaha ili kukabili msongo wa mawazo limekuwa gumzo wakati wa mazishi ya Caroline Kangogo. Ni hali ambayo imewakumba wengi. Je, lipi lifanyike ili kukabili hali hii? Aidha, kila kiongozi wa NASA sasa anautoroka muungano huo. Kunani? Na baada ya hatua hiyo, wataingia katika miungano gani au nani ataungana na nani? Raila pia amejaribu kujitangaza Mlima Kenya kupitia wanamiziki, wafanyabiashara na baadhi ya wanasiasa. Je, atabadili nyoyo za wakazi wa huko ambao...
Published 07/31/21
Cheche kali za maneno zinaendelea ndani ya Jubilee baada ya kurambishwa sakafu na UDA huko Kiambaa, huku baadhi wakishinikiza kufurushwa kwa Tuju na Murathe chamani. Kenyatta naye amefoka akiwa Kilifi na kuwataja kuwa maadui wanaotatiza juhudi zake za kuleta umoja na maendeleo. Je, hao maadui ni akina nani? Vipi kuhusu reggae ya BBI? Kenyatta na Odinga wasisitiza kwamba ngoma hiyo ingalipo na kwamba marekebisho ya katiba yatafanyika. Wana njia gani mbadala ya kufanikisha lengo hilo? Huko...
Published 07/25/21
Raila Odinga ameandika maono 15 ambayo angependa kuafikiwa nchini. Ruto na Mudavadi wamemsuta wakisema anashtukia mambo ambayo wengine wamekuwa wakiyazungumzia. Mbali na hilo, Raila anadai hakusema kwamba likuwa na risasi moja ya kuwania urais. Pia akiulizwa, anasema hajatangaza iwapo atawania. Je, unamwamini? Raila pia anasema kura ya maamuzi lazima ifanyike, hata miezi 3 kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022. Suala jingine ni hatua ya Uhuru kuzindua usiku huduma za afya Nairobi, huku akieleka...
Published 07/13/21
Mapambano ya kisheria yamedhihirika katika Mahakama ya Rufaa. Hoja kuu ikiwa mwasisi hasa wa BBI ni nani. Ni Rais Kenyatta, Raila Odinga au ni Junet Mohammed na Dennis Waweru? Aidha, ripoti ya Mhasibu Mkuu wa Serikali imeweka wazi jinsi wabunge wanavyopora pesa za umma kupitia marupurupu ya usafiri. Pia, serikali inaendeleza kopakopa na mara hii Rais amekwenda kuomba bilioni 160 nchini Ufaransa huku serikali ikikosa kutii agizo la IMF kwamba ichapishe majina ya Covid-19 billionairs....
Published 07/04/21
Suala la viongozi wote kutakiwa kuwa na digrii ili kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa limezua gumzo nchini huku Naibu wa Rais, William Ruto akiungana na wanaopinga hitaji hilo lililotajwa na IEBC. Tayari Seneta Kipchumba Murkomen ameandaa mswada unaolenga kufutilia mbali hitaji hilo huku watakaowania wakitakiwa kuwa na uwezo wa kusoma na kuandika lugha za Kiswahili na Kiingereza pekee na wenye mahitaji maalumu kujua lugha ya ishara. Je, uongozi unategemea kiwango cha masomo? Aidha, Rais...
Published 06/24/21
Hisia kali zimejitokeza kufuatia bajeti iliyosomwa na Waziri wa Fedha, Ukur Yattani huku Wakenya wakilalamikia kukandamizwa kwani watazidi kutozwa kodi ya juu ili kufadhili bajeti hiyo ya shilingi trilioni 3.6. Wakulima nao wanalalamikia kukandamizwa kwa sekta ya kilimo ilhali ni uti wa mgongo wa taifa hili. Vilevile, Wakenya wameghadhabishwa na kauli ya Waziri Yattani kwamba serikali itaendelea kukopa kwani watatozwa kodi zaidi. Aidha, mashinikizo yanazidi kutolewa kwa Rais Kenyatta...
Published 06/13/21
Hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kuwaidhinisha majaji 34 na kuwaacha 6 akiwamo, Joel Ngugi na George Odunga ambao walikuwa miongoni mwa majaji walioharamisha BBI, imeendelea kuibua hisia kinzani hasa kuhusu uhuru wa Idara ya Mahakama. Je, unadhani Rais analipiza kisasi ama kuna sababu maalumu za kuwakataa sita hao? Aidha, katika maadhimisho ya Madaraka, Rais aliendelea kushtumu mahakama akisema majaji wanatoa uamuzi bila kujali athari zake kiuchumi. Je, unafikiri majaji wanatumia sheria kuhujumu...
Published 06/08/21
Mjadala mkali unaendelea kuhusu iwapo mchakato wa BBI unafaa kusitishwa kabisa hadi baada ya uchaguzi mkuu ujao au la. Naye Naibu wa Rais, William Ruto amesema kusimamishwa kwa BBI mahakamani vilevile mikutano ya kisiasa ni ujumbe kwamba pana haja ya mashauriano kufanyika kuhusu mustakabali wa Kenya. Aidha, Kenyatta amezindua upya Kiwanda cha Nyama, KMC chini ya Jeshi la Ulinzi KDF, akisema anategemea sana KDF katika kutekeleza maendeleo kwa sababu ya bidii, uwajibikaji na bajeti yake nafuu...
Published 05/30/21
Wakenya wanatoa hisia kali kuhusu chaguzi ndogo za Bonchari, Juja na Rurii ambapo polisi wengi walionekana, suala ambalo wengi hata viongozi walilalamikia vikali. Aidha, kung'aa kwa UDA na kushindwa kwa Jubilee katika chaguzi ndogo kumechochea mjadala nchini. Jambo jingine ni je, Mahakama ya Rufaa pia itaangusha BBI au la? John Mbuthia wa Nyeri, William Omasire wa Nyamira na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na Wakenya kuhusu masuala haya.
Published 05/26/21
Kufuatia madai mengi kwamba waendesha-bobaboda wanaongoza katika kushiriki mapenzi na wasichana pia wanawake walioolewa, tumezungumza na baadhi yao kujua kama ni kweli, vilevile kulenga kujua sababu. Wanakiri, huku wakisema wanawake wenyewe ndio huwatongoza. Mmoja wao anakiri kujihusisha na zaidi ya wanawake 80. Sikiliza mazungumzo baina yao na wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Willie Khaemba wa Bungoma na Martin Ndiema wa Kitale.
Published 05/19/21
Wakenya wametoa hisia mbalimbali kufuatia hatua ya Mahakama Kuu kusitisha mchakato wa marekebisho ya katiba kupitia BBI. Majaji watano wa mahakama hiyo wanasema kuwa Rais Kenyatta alivunja sheria kwa kuanzisha mchakato huo; kwamba haukuanzishwa na wananchi wala bunge jinsi inavyosema katiba. Kamati-simamizi ya BBI inakata rufaa. Je, Reggae itarejelewa au la? Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraese wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na Wakenya...
Published 05/15/21
Wakenya wanailaumu serikali kwa kuchukua mikipo mara kwa mara. Aidha wanaulaumu kwa kutoweka mikakati ya kuwainua kiuchumi kutokana na athari za korona. Wanahabari wetu wa Nyeri, John Mbuthia, Moses Kiraese wa Pokot na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wamezungumza na wakazi wa maeneo yao.
Published 04/18/21
Barua Kang'ata Yatetemesha! ​
Published 01/22/21
Gumzo la Maisha - Episode 1
Published 12/24/20