GUMZO LA WIKI PODCAST: Mauaji Yamezidi, Nao Wanasiasa Wamechanganyikiwa
Listen now
Description
Suala la polisi kupewa ushauri nasaha ili kukabili msongo wa mawazo limekuwa gumzo wakati wa mazishi ya Caroline Kangogo. Ni hali ambayo imewakumba wengi. Je, lipi lifanyike ili kukabili hali hii? Aidha, kila kiongozi wa NASA sasa anautoroka muungano huo. Kunani? Na baada ya hatua hiyo, wataingia katika miungano gani au nani ataungana na nani? Raila pia amejaribu kujitangaza Mlima Kenya kupitia wanamiziki, wafanyabiashara na baadhi ya wanasiasa. Je, atabadili nyoyo za wakazi wa huko ambao wamekuwa wakimwogopa? Wanahabari John Mbuthia, William Omasire na Martin Ndiema wanatupambia makala haya.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu...
Published 11/05/22