Gumzo la Wiki Podcast; Usalama wa Ruto - Wakenya wazungumza
Listen now
Description
Suala la usalama wa Naibu wa Rais, William Ruto limezua mjadala mkali wiki hii na hata kugeuka kuwa mazungumzo ya kulinganisha mali anayomiliki Ruto dhidi ya viongozi wengine. Aidha, maswali mengi yameibuliwa kufuatia jinsi Waziri wa Usalama, Dkt. Fred Matiang'i alivyotumia vikao vya bunge kutangaza mali ya Ruto hasa inayolindwa na maafisa wa usalama. Je, unadhani hatua hiyo imemmaliza au ndiyo imemjenga Ruto kisiasa? Vilevile siasa za Mlima Kenya zinazidi kushika kasi huku baadhi ya viongozi wakisema Raila anatosha licha ya kufikirika kuachwa na Uhuru kujitafutia kura mlimani. Si hayo tu, Waziri wa Elimu Prof. Geoge Magoha anasema mzazi ambaye mwanawe hajaenda shuleni atakamatwa. Wanahabari wetu; John Mbuthia wa Nyeri na Moses Kiraise wa Pokot Magharibi wametangamana na wananchi kupata hisia zao katika makala haya.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu...
Published 11/05/22