GUMZO LA WIKI PODCAST; Rais anahujumu idara ya mahakama, Wakenya wazungumza
Listen now
Description
Hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kuwaidhinisha majaji 34 na kuwaacha 6 akiwamo, Joel Ngugi na George Odunga ambao walikuwa miongoni mwa majaji walioharamisha BBI, imeendelea kuibua hisia kinzani hasa kuhusu uhuru wa Idara ya Mahakama. Je, unadhani Rais analipiza kisasi ama kuna sababu maalumu za kuwakataa sita hao? Aidha, katika maadhimisho ya Madaraka, Rais aliendelea kushtumu mahakama akisema majaji wanatoa uamuzi bila kujali athari zake kiuchumi. Je, unafikiri majaji wanatumia sheria kuhujumu serikali ama ni serikali ndiyo inayokiuka katiba? Si hayo tu, Rais Kenyatta amekosolewa vikali baada ya kuzindua miradi kwenye eneo la Nyanza. Je, anafanya maendeleo kwa ubaguzi? Wanahabari wetu Moses Kiraise wa Pokot Magharibi, William Omasire wa Nyamira na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wananchi kuhusu masuala haya.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22