GUMZO LA WIKI PODCAST; BBI iendelee au la? Uhuru ataacha rekodi ya maendeleo? Wakenya wanajadili
Listen now
Description
Mjadala mkali unaendelea kuhusu iwapo mchakato wa BBI unafaa kusitishwa kabisa hadi baada ya uchaguzi mkuu ujao au la. Naye Naibu wa Rais, William Ruto amesema kusimamishwa kwa BBI mahakamani vilevile mikutano ya kisiasa ni ujumbe kwamba pana haja ya mashauriano kufanyika kuhusu mustakabali wa Kenya. Aidha, Kenyatta amezindua upya Kiwanda cha Nyama, KMC chini ya Jeshi la Ulinzi KDF, akisema anategemea sana KDF katika kutekeleza maendeleo kwa sababu ya bidii, uwajibikaji na bajeti yake nafuu ikilinganishwa na zile za wanakandarasi wengine. Je, Rais Kenyata ataacha rekodi gani ya uongozi ikizingatiwa kwamba mahakama imekuwa ikitoa maamuzi ya kuharamisha mipango yake ukiwamo uhamisho wa KMC kutoka Wizara ya Kilimo hadi KDF? Wanahabari wetu, Moses Kiraise wa Pokot Magharibi, Robert Menza wa Mombasa na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wananchi katika makala haya.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22