Description
Suala la viongozi wote kutakiwa kuwa na digrii ili kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa limezua gumzo nchini huku Naibu wa Rais, William Ruto akiungana na wanaopinga hitaji hilo lililotajwa na IEBC.
Tayari Seneta Kipchumba Murkomen ameandaa mswada unaolenga kufutilia mbali hitaji hilo huku watakaowania wakitakiwa kuwa na uwezo wa kusoma na kuandika lugha za Kiswahili na Kiingereza pekee na wenye mahitaji maalumu kujua lugha ya ishara.
Je, uongozi unategemea kiwango cha masomo?
Aidha, Rais Kenyatta amesema yu tayari kumuunga mkono mgombea wa NASA suala ambalo limempandisha hasira Ruto. Isitoshe, Kalonzo ameapa kutokuwa mgombea mwenza wa Raila, huku akiambiwa aache kubweka.
Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri na Moses Kiraese wa Pokot Magharibi wamewashirikisha Wakenya katika gumzo. hili.