Gumzo la Wiki Podcast; Kweli, twachangia mimba na kuvunja ndoa - waendesha bodaboda wakiri
Listen now
Description
Kufuatia madai mengi kwamba waendesha-bobaboda wanaongoza katika kushiriki mapenzi na wasichana pia wanawake walioolewa, tumezungumza na baadhi yao kujua kama ni kweli, vilevile kulenga kujua sababu. Wanakiri, huku wakisema wanawake wenyewe ndio huwatongoza. Mmoja wao anakiri kujihusisha na zaidi ya wanawake 80. Sikiliza mazungumzo baina yao na wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Willie Khaemba wa Bungoma na Martin Ndiema wa Kitale.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu...
Published 11/05/22