Gumzo la Wiki; Wakenya Kuhusu Mahakama kusimamisha BBI
Listen now
Description
Wakenya wametoa hisia mbalimbali kufuatia hatua ya Mahakama Kuu kusitisha mchakato wa marekebisho ya katiba kupitia BBI. Majaji watano wa mahakama hiyo wanasema kuwa Rais Kenyatta alivunja sheria kwa kuanzisha mchakato huo; kwamba haukuanzishwa na wananchi wala bunge jinsi inavyosema katiba. Kamati-simamizi ya BBI inakata rufaa. Je, Reggae itarejelewa au la? Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraese wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na Wakenya kuhusu suala hili.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu...
Published 11/05/22