Gumzo la Wiki Podcast: Wakenya wakosoa bajeti; haimjali mtu wa kawaida
Listen now
Description
Hisia kali zimejitokeza kufuatia bajeti iliyosomwa na Waziri wa Fedha, Ukur Yattani huku Wakenya wakilalamikia kukandamizwa kwani watazidi kutozwa kodi ya juu ili kufadhili bajeti hiyo ya shilingi trilioni 3.6. Wakulima nao wanalalamikia kukandamizwa kwa sekta ya kilimo ilhali ni uti wa mgongo wa taifa hili. Vilevile, Wakenya wameghadhabishwa na kauli ya Waziri Yattani kwamba serikali itaendelea kukopa kwani watatozwa kodi zaidi. Aidha, mashinikizo yanazidi kutolewa kwa Rais Kenyatta kuwaapisha majaji sita ambao aliwaacha nje wakati wa uteuzi wake. Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Faith Kutere wa Uasin Gishu na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na Wakenya kuhusu masuala haya.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22