Gumzo la Wiki Podcast: Ziara ya Ruto Uganda - cheche za ODM na NRM; kauli za Wakenya
Listen now
Description
Suala la kuzuiwa kwa Ruto kwenda Uganda linazidi kuzua gumzo, taifa hilo likisema halikufahamu kuhusu ziara hiyo. Karanja Kibicho naye anasema ofisi yake haikuwa na habari. Nani hasa aliyepiga simu Ruto azuiwe? ODM nayo inasema Ruto alilenga kwenda Uganda kujifunza namna ya kutwaa uongozi kwa nguvu ama kukatalia madaraka. Je, bottom up ni ya kuinufaisha Uganda jinsi inavyodai ODM? Naye Murathe amewasisitizia Wakenya kwamba Raila ndiye atakayekuwa Rais 2022. Murathe anajua siri gani ya kufanikisha hilo? Na je, Raila atakubaliwa Mlima Kenya? Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraese wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wametangamana na wananchi kuhusu masuala haya.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu...
Published 11/05/22