GUMZO LA WIKI PODCAST: Kivumbi cha chaguzi ndogo, vilevile BBI; Wakenya wanasemaje?
Listen now
Description
Wakenya wanatoa hisia kali kuhusu chaguzi ndogo za Bonchari, Juja na Rurii ambapo polisi wengi walionekana, suala ambalo wengi hata viongozi walilalamikia vikali. Aidha, kung'aa kwa UDA na kushindwa kwa Jubilee katika chaguzi ndogo kumechochea mjadala nchini. Jambo jingine ni je, Mahakama ya Rufaa pia itaangusha BBI au la? John Mbuthia wa Nyeri, William Omasire wa Nyamira na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na Wakenya kuhusu masuala haya.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu...
Published 11/05/22