GUMZO LA WIKI PODCAST: Jubilee imesambaratika? Mpango mbadala wa BBI ni gani?
Listen now
Description
Cheche kali za maneno zinaendelea ndani ya Jubilee baada ya kurambishwa sakafu na UDA huko Kiambaa, huku baadhi wakishinikiza kufurushwa kwa Tuju na Murathe chamani. Kenyatta naye amefoka akiwa Kilifi na kuwataja kuwa maadui wanaotatiza juhudi zake za kuleta umoja na maendeleo. Je, hao maadui ni akina nani? Vipi kuhusu reggae ya BBI? Kenyatta na Odinga wasisitiza kwamba ngoma hiyo ingalipo na kwamba marekebisho ya katiba yatafanyika. Wana njia gani mbadala ya kufanikisha lengo hilo? Huko Nyanza, tabia ya Wakenya ya kujihatarisha kwa kuchota mafuta imedhihirika tena. Je, mbona hawajifunzi kutokana na mikasa ya awali? Wanahabari wetu, Rose Mukonyo wa Machakos, Willie Khaemba wa Bungoma na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wakazi na kutupambia makala ya leo.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu...
Published 11/05/22