GUMZO LA WIKI PODCAST: Kuchanganyikiwa ndani ya NASA; Raila na Kalonzo walumbana
Listen now
Description
Raila Odinga ameandika maono 15 ambayo angependa kuafikiwa nchini. Ruto na Mudavadi wamemsuta wakisema anashtukia mambo ambayo wengine wamekuwa wakiyazungumzia. Mbali na hilo, Raila anadai hakusema kwamba likuwa na risasi moja ya kuwania urais. Pia akiulizwa, anasema hajatangaza iwapo atawania. Je, unamwamini? Raila pia anasema kura ya maamuzi lazima ifanyike, hata miezi 3 kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022. Suala jingine ni hatua ya Uhuru kuzindua usiku huduma za afya Nairobi, huku akieleka Ukambani mchana kuzindua miradi. Mbona asizindue miradi yote usiku ikizingatiwa kuwa korona ingalipo? Kwa uhondo kamili kuhusu masuala haya, wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri, William Omasire wa Nyamira na Martin Ndiema akiwa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wakazi wa maeneo hayo.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu...
Published 11/05/22